Dk. Mwinyi aliyasema
hayo, Ikulu, Zanzibar alipozungumza na uongozi wa taasisi ya kiraia,
inayounganisha Jumuiya za wanawake kutoka vyama mbalimbali vya siasa vyenye
usajili kamili nchini, tasisi ya Sauti ya wanawake wenye ulemavu (SWAUTA),
Chama cha wabunge wanawake (TWPG) na Umoja wa wanawake wa Baraza la Wawakili
(UWAWAZA). T-WCP - ULINGO. Waliofika kumkabidhi tunzo ya hongera kwa mafaniko makubwa
aliyofanya ndani ya muda mfupi wa uongozi wake.
Alisema serikali zote
mbili zitaendelea kutoa fursa za kutosha kwa wanawake kwenye maeneo mbalimbali
ili kutekeleza azma yao kufikia 50 kwa 50.
Alisema maendeleo
yana taka kwa usawa wakijinsia kutoa haki na fursa sawa katika maendeelo
ikiwemo elimu, afya na jamii kwani kumuelemisha mwanamke kutaondoa changamoto
nyingi kwenye jamii
“Sijajuta hata kidogo
kwa wale wanawake niliowateua kwenye Serikali yangu, kwa kweli naona umuhimu wa
kuwaongeza kwenye safu mbalimbali” Alibainisha Rais Dk. Mwinyi.
Aidha, alisema Serikali
pia itaendelea kuimarisha huduma za mama na mtoto ili kupunguza changamoto
nyingi kwa wanawake.
Rais Dk. Mwinyi pia aliwapongeza
ULINGO kwa kazi kubwa wanayoifanya kuunganisha pamoja sauti ya pamoja, na
kuwasifu hatua yao ya kutanguliza maslahi mapana ya taifa kwa kuunganisha nguvu
ya umoja wao bila kujali tofauti ya itikadi zao za kisiasa pamoja na
kuwashirikisha wanawake wengi na kuwashajihisha kitaaluma kujua haki na wajibu
wao kwenye masuala haki na siasa.
Alisema, katiba ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki kwa jinsia zote kushiriki katika
masuala siasa. Pia Dk. Mwinyi aliahidi kuipokea tunzo hiyo kama sehemu ya
kuongeza za kuweka fursa sawa za jinsia kwenye maeneo yote.
Nao, viongozi wa
taasisi hiyo wamempongeza Dk. Mwinyi kwa kutekeleza kwa vitendo masuala ya
usawa wa kijinsia na ujumuishi wa makundi maalum katika ngazi mablimbali za
maamuzi, kulinda na kudumisha amani, umoja na utulivu nchini na kushajihisha
umoja wa kitaifa pamoja na masuala ya msingi kwa maendeleo endelevu.
Pia, walimpongeza
Rais Dk. Mwinyi kwa kutambua kikwazo kimubwa kinachowanyima fursa wananwake
ikiwemo ukosefu wa elimu, changamoto kwenye sekta ya afya kwa kuweka
miundombinu imara ili kukabiliana na changamoto pamoja na huzitatua kwa kipindi
kifupi cha uongozi wake.
Akizungumza kwenye
halfa hiyo kwa niaba ta Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Anna Magareth Abdalla,
Makamo Mwenyekti wa taasisi hiyo kwa Zanzibar ambae pia ni Naibu Spika wa
Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan alimuahidi Dk. Mwinyi mwaka 2025
atarejeshwa tena madarakani kwa nguvu na umoja wa wanawake nchini ambao kwasasa
sauti yao ni moja tu ya kudumisha amani yanchi na maendeleo kwa maslahimapana
ya taifa.
Pia alitumia fursa
hiyo kumpongeza Dk. Mwinyi kwa kwa mageuzi makubwa aliyoiletea Zanzibar kupitia
sekta za Afya, Elimu na Uchumi wa Buluu pamoja na kuongeza fursa za uongozi na
maendeleo kwa wanawake na kumuahidi daima wanamuunga mkono katika kuiletea maendeleo
makubwa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment