RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akizungumza na mgeni wake Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe.Regine Hess,
mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, alipofika
kwa mazungumzo na kumuaga leo 8-6-2023
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya
uwekezaji ni muhimu katika ustawi wa uchumi wa Zanzibar.
Dk. Mwinyi aliyasema
hayo, Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania,
Regine Hess aliefika kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa
utumishi hapa Tanzania.
Alisema, Zanzibar
bado ina fursa pana ya kuendelea kunufaika na uwekezaji kutoka Ujerumani kutokana
na ushirikiano mwema ulipo baina yao.
“Bado tuna fursa
kubwa ya kuendelea kushirikiana na Ujerumani katika kukuza uwekezaji na
kuongeza watalii wengi, Zanzibar. Tunashajihisha sana suala la uwekezaji sababu
ndio kiungo kikubwa kwa uchumi wa Zanzibar” Alifafanua Dk. Mwinyi.
Rais Dk. Mwinyi alieleza,
Ujerumani imetoa mchango mkubwa kwa kuiinga mkono Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kupitia sekta ya maji safi na salama ambayo aliieleza kuwa ni sekta
muhimu kwa ustawi wa watu wa Zanzibar.
Pia Dk. Mwinyi aliishikuru
Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano wanaendelea kuutoa kwa SMZ kupitia Sekta ya
Afya na Michezo pamoja na kushajihisha watalii wengi raia wa Ujerumani
wanaoingia Tanzania.
Akizungumza kwenye
hafla hiyo, Balozi Hess alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa weledi wake wa
kuridhia uongozi wake wa Serikali ya Umoja wa kitaifa pamoja na hatua
alizozichukua za kuunda kamati ya maridhiano kitaifa kati ya Chama tawala CCM
na cha upinzani ACT Wazalendo, akimsifu kwa jitihada zake za kuendelea
kudumisha amani na utulivu wa kisiasa, Zanzibar.
Wakati huo huo, Balozi
Hess alimtambulisha kwa Rais wa Zanzibar, Balozi wa heshima Dk. Jenny Bouraima atakaeiwakilisha
Ujerumani na kufanya kazi zake hapa Zanzibar.
Akizungumza mara bara
baada ya utambulisho huo, Dk. Jenny ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zaznzibar
na kuahidi kushirikiana nayo bega kwa bega hasa kwenye suala zima la kuitangaza
zaidi Zanzibar kupitia sekta ya utalii pamoja na kuiunga mkono sera ya Uchumi
wa Buluu kwa kuwashajihisha zaidi Wajerumani kuja Zanzibar kuwekeza kupitia
rasilimali bahari.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiwa katika mazungumzi na mgeni wake Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe.Regine
Hess, alipofika Ikulu kwa mazungumza na kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi
Nchini Tanzania, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini
Zanzibar leo 8-6-2023 na (kushoto kwa Rais)Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akizungumza na mgeni wake Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe.Regine Hess,
mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, alipofika
kwa mazungumzo na kumuaga leo 8-6-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya picha mgeni wake Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe.Regine Hess, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 8-6-2023, alipofika kwa ajili ya mazungumzo na kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini TanzaniaRAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiagana na mgeni wake Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe. Regine Hess,
baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini
Zanzibar leo 8-6-2023. Alipofika kwa ajili ya mazungumzo na kumuaga baada ya
kumaliza muda wake wa Kazi Nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment