Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan afunga Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha kwa Mfipa Mkoani Pwani tarehe 27 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali wakati akifunga Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani tarehe 27 Agosti, 2023.
Wakuu wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akifunga Mafunzo yao yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha kwa Mfipa Mkoani Pwani tarehe 27 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Tamisemi Mhe. Angellah Kairuki katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa mara baada ya kufunga mafunzo yao katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha kwa Mfipa Mkoani Pwani tarehe 27 Agosti, 2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.