Habari za Punde

Wagombea 58 Wateuliwa Kuwania Ubunge na Udiwani

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbarali Bw.Missana Kwangura akibandika fomu za uteuzi za vyama kumi na tatu vilivyoteuliwa kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbarali mkoani Mbeya. Wagombea hao walioteuliwa majina yao na vyama katika mabano ni Halima Magambo (AAFP), Osward Mndeva (DP), Zavely Seleka (UDP), Exavery Mwataga (CCK), Mary Daudi (UPDP), Modestus Kilufi (ACT WAZALENDOazalendo), Morris Nkongolo (TLP), Hashim Mdemu (ADC), Fatuma Ligania (NLD), Mwajuma Milambo (UMD), Bahati Ndingo (CCM), Husseni Lusewa (ADA-TADEA) Bariki Mwanyalu (DEMOKRASIA MAKINI). 
Baadhi ya wagombea na wananchi wakiangalia fomu za wagombea walioteuliwa kuwania Kiti cha Ubunge jimbo la Mbarali. 
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Nala, Judith Kwaleka akibandika fomu za uteuzi za wagombea 11 Kati ya 13 waliochukua fomu za uteuzi kuwania nafasi ya udiwani katika Kata hiyo ya Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Wagombea walioteuliwa Leo Agosti 19,2023 majina yao na vyama vyao katika mabano ni Helman Masila (CCM), Sito Malugu ( ACT Wazalendo), Asha Kijuu ( UMD), Hawa Said (SAU), Marijan Mtugani (ADC), Eva Kaka ( AAFP),  Godfrey Maguhwa (ADA-TADEA), Baraka Machumu ( Demokrasia Makini), Abuutwahiru Idd (CCK), Mwanahamisi Mhando ( TLP) na Mohamed Mnyalape (NCCR Mageuzi). Uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya na Madiwani katika Kata sita za Tanzania bara unaotaraji kufanyika Septemba 19,2023.
Wagombea na wafuasi wao wakiangalia fomu za uteuzi zilizowekwa wazi na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Uteuzi ulifanyika Agosti 19,2023 ambapo uchaguzi katika Jimbo la Mbarali na Kata sita za Tanzania bara unataraji kufanyika Septemba 19 mwaka huu
*****************
Wagombea 58 kutoka vyama 17 vya siasa vyenye usajili kamili wameteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwania nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo la Mbarali lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na kata sita za Tazanzania Bara.

Tarehe 05 Agosti, 2023 Tume ilitangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara na uteuzi wa wagombea umefanyika tarehe 19 Agosti, 2023, kampeni zimeanza tarehe 20 Agosti 2023 na zinatarajiwa kuhitimishwa tarehe 18 Septemba, 2023 ambapo uchaguzi utafanyika tarehe 19 Septemba, 2023.

Fomu za uteuzi wa wagombea zilitolewa kuanzia tarehe 13 hadi 19 Agosti, 2023 ambapo jumla ya wagombea 70 walichukua fomu.

Kati ya wagombea 70 waliochukua fomu, wanawake walikuwa 21 na wanaume walikuwa 49. Kati ya wagombea 58 walioteuliwa wanawake ni 14 na wanaume ni 44.
 
Wagombea hao wametoka kwenye vyama 17 ambavyo ni; CCM, AAFP, ACT – WAZALENDO, TLP, NRA, SAU, ADA – TADEA, ADC, CCK, CUF, DEMOKRASIA MAKINI, DP, NCCR – MAGEUZI, NLD, UDP, UMD na UPDP.
 
Kata zitakazofanya uchaguzi mdogo ni; Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, mkoani Dodoma, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi na Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.