Habari za Punde

KVZ Yaibuka na Ushindi Bao 2-0 Dhidi ya Timu ya Finya

Na.Mwandishi Wetu Zanzibar.

MAAFANDE wa timu ya KVZ wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Maendeleo katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliochezwa uwanja wa Finya kisiwani Pemba. 

Mchezo huo uliokuwa ulianza Kwa mashambulizi ya kushtukiza na KVZ kufanikiwa kupata bao dakika ya nne lililofungwa na Saad Khalfan Kipanga, bao ambalo lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza na KVZ kama kawaida yake ikaongeza mashambulizi na kufanikiwa kuongeza bao la pili na la ushindi lililofungwa na Suleiman Mwalimu dakika ya 51.

Wakati Pemba matokeo yakiwa hayo, lakini katika kiwanja Cha Mao Zedong A timu za kmkm na uhamiaji zimeshindwa kutambiana baada ya kutokea sare tasa.

Ligi hiyo itaendelea tena jumapili ya Septemba 17 kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha JKU na New City.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.