Mkuu wa Divisheni ya utawala Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Abdulla Mohammed Haji akiuliza suali kwa maofisa wa ZHSF wakati wakipatiwa taarifa ya hali ya usajili wa wafanyakazi katika Mfuko wa Huduma za Afya huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO
Na Takdiri Ali Maelezo
Maafisa utumishi naTehama wa taasisi za Serikali wameshauriwa kufuata taratibu zilizowekwa na Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) ili kukamilisha usajili wa Wafanyakazi katika Mfuko huo kwa ufanisi na kwa wakati uliokusudiwa.
Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Yaasin Ameir Juma wakati alipokuwa akizungumza na maofisa hao katika kikao kazi kilichofanyika Ukumbi wa Studio Rahaleo.
Amesema mfuko ulitarajia kusajili wafanyakazi elfu hamsini kabla ya Oktoba na hadi sasa jumla ya wafanyakazi 36347 wamekamilisha usajili huo.
Kutokana na hali hiyo Mfuko umeamua kukaa na Maafisa hao kujadiliana juu ya changamoto zinazopelelekea kuzorota kwa usajili huo na kuzipatia ufumbuzi.
Mkuu huyo Amewataka Maofisa Tehama kufuata utaratibu uliowekwa na Mfuko ili kuondosha usumbufu unaojitokeza ikiwemo kukataa kwa mfumo huo mara wanapoingiza taarifa za Mfanyakazi zisizo sahihi.
Aidha amesema malengo ya ZHSF ni kutoa huduma za Afya kwa Wanachama wake ifikapo Oktoba mwaka huu hivyo aliwataka Maofisa hao kuwasaidia wafanyakazi kujisajili ili kukamilisha zoezi hilo kwa wakati na kufikia malengo ya Serikali.
Awali aliwataka Maafisa hao kushirikiana na Watendaji wa Mfuko ili kurahisha kukamilika kwa zoezi hilo kwa haraka kama ilivyokusudiwa.
Nao Maofisa hao wameushauri Uongozi wa Mfuko kuweka dawati maalum la kusikiliza changamoto za wateja wao na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.
Aidha waliushauri Mfuko wa huduma za Afya kuandaa mazingira ya kufuatilia na kuzidhibiti baadhi ya hospitali ambazo zimekua na Tabia ya kuwaongezea maradhi wasiokuwanayo kwa maslahi binafsi.
“Unaenda hospitali unaumwa na kichwa tu utaandikiwa vipimo vyote vikubwa na dawa unazopewa nying
No comments:
Post a Comment