Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Bi. Asya Iddi Issa, ameshiriki katika ghafla fupi ya kumuaga Mwalimu Mkuu Mstaafu wa Skuli ya K/Samaki A Islamic Ndugu Maalim Mussa Abdi Khamis.
Katika hafla hiyo Mkurugenzi Asya ametumia fursa hiyo kwa kuwanasihi Walimu kuongeza mashirikiano na kuchukua mazuri yote yaliyoachwa na Mwalimu Mkuu Mstaafu.
Aidha, Amewataka Walimu hao kuongeza bidii na kasi katika ufundishaji kwa wanafunzi ili adhma ya utowaji wa Elimu bora iweze kufikiwa.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA )
Tarehe: 28/10/2023
No comments:
Post a Comment