Habari za Punde

PBZ yakabidhi vitendea kazi kwa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar

Mkuu wa habari na Mawasiliano Mohamed Mansour kutoka Taasisi ya Afisi ya Rais,Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini(PDB) akizungumza na wakuu wa PBZ na Maafisa Habari kutoka Habari Maelezo baada ya makabidhiano ya vitendea kazi vilivyotolewa na PBZ ili kuboresha utandaji kazi wa idara hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji Benki ya watu wa Zanzibar DK. Muhusini Salum Masoud   akizungumza na maafisa  wa Idara ya Habari Maelezo wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi vilivyotolewa na PBZ ili kuboresha utandaji kazi wa idara hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Asha Juma Khamis akipokea vifaa kwaajili ya kuboresha utendaji kazi wa idara hiyo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji Benki ya watu wa Zanzibar PBZ  DK Muhusini Salum  Masoud   Mpirani Mjini Unguja.

Picha na Fauzia Mussa HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Sheha Haji Sheha,   Maelezo                       27 october 2023

Benki ya watu wa Zanzibar imekabidhi vifaa mbali mbali kwa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar ili kuboresha  utendaji  kazi wa idara hiyo.    

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo  Mkurugenzi mtendaji PBZ Dk.Muhsin Salim Masoud alisema vifaa hivyo vitaondoa upungufu wa vitendea kazi katika Ofisi hiyo.

Hata hivyo amesema  PBZ itakua mbele muda wowote kuuunga mkono jitihada za Idara hiyo  katika kuhakikisha inaendelea kufikisha taarifa za utendaji wa Serikali kwa jamii.

Aidha amesema PBZ imetoa vifaa hivyo ikiwa ni mwendelezo wao  wa kujenga mahusiano mema na taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi ili kuona zinatekeleza  majukumu yao   kwa ufanisi.

Sambamba na hayo alisema kuelekea maadhimsho ya miaka 60 ya Mapinduzi Benki hiyo  inatarajia kuzindua miradi mbalimbali inayolenga kuboresha huduma za benki kwa jamii.

Akifafanua baadhi ya miradi hiyo alisema ni  pamoja na ufunguzi wa  Tawi la Malindi, Forodhani, Mlandege, Amani Nungwi, Morogoro, Mbeya, Michenzani pamoja na uzinduzi wa mfumo mpya wa Mobile na internet benki.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Asha Juma Khamis alisema vifaa hivyo ni njia moja wapo itakayopelekea wafanya kazi kutekeleza majukumu yao ya kufikisha  taarifa  kwa jamii kwa wakati.

Pia ameishukuru PBZ kwa kushirikiana na Taasisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini PDB katika kufanikisha upatikanaji wa vifaa hivyo vinavyoenda kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji katika Idara hiyo,na kuahidi kuvitunza na kuvifanyia kazi zilizokusudiwa.

Naye Mkuu wa habari na Mawasiliano kutoka (PDB) Mohamed Manssor aliwataka Maafisa wa Idara ya Habarai maelezo  kuhakikisha wanavifanyia kazi iliyokusudiwa ili kufikia malengo ya Serikali katika Idara hiyo.

 Katika makabidhiano hayo Idara ya habari Maelezo ilipokea  vifaa mbali mbali vya kiutendaji ikiwemo Laptop na  Scaner.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.