Habari za Punde

Waziri Tabia azindua mradi wa kukuza maendeleo ya jamii

kuu wa Ofisi na Mwakilishi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO  Michel Toto akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa kukuza maendeleo  ya kijamii (Alwaleed Philanthropies Project) kupitia elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayohusiana na utamaduni (TVET) na ajira wakati wa uzinduzi wa mradi huo huko Verde Mjini Unguja.
Waziri wa Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita  akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuzindua  mradi wa kukuza maendeleo  ya kijamii (Alwaleed Philanthropies Project) kupitia elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayohusiana na utamaduni (TVET) na ajira chini ya ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),huko Verde Mjini Unguja.

Waziri wa Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza wakati akizindua  mradi wa kukuza maendeleo  ya kijamii (Alwaleed Philanthropies Project) kupitia elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayohusiana na utamaduni (TVET) na ajira chini ya ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),huko Verde Mjini Unguja.


Na Fauzia Mussa,   Maelezo

 

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita  amesema kuwepo kwa miradi ya kukuza maendeleo ya jamii kupitia ujasiriamali kutaongeza na kuzalisha ajira kwa Vijana.

 

 Akizungumza wakati  akizindua mradi wa kukuza maendeleo ya kijamii kupitia elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayohusiana na utamaduni (TVET) na ajira huko Verde Waziri Tabia amesema  hatua hiyo itaongeza ubunifu wa kazi za sanaa na kurahisisha upatikanaji wa masoko ya kazi hizo .

 

Amesema Vijana wengi wa Zanzibar wanajishuhulisha na kazi za sanaa na utamaduni ikiwemo uchongaji,uchoraji  na muziki asilia hivyo Wizara itakua mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za mradi huo ili kufikia malengo yaliokususdiwa.

 

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Bakari   Ali Silima amesema  mradi huo umekuja wakati muafaka na utaongeza kasi ya utekelezaji wa mabadiliko ya elimu ambapo Wizara inakusudia   kuifanya elimu ya amali kuwa ya lazima baada ya kukamilika kwa marekebisho ya sheria ya elimu ya  mwaka 1982 na sera ya mwaka  2006.

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na  Michezo Tanzania Nicolas Mkapa amesema mradi huo unaendana na matakwa halisi ya ajira kufuatia mageuzi ya mitaala ya elimu yanayotoa kipaombele katika stadi za kazi ili kukuza sanaa , ubunifu na tija .

 

Akitolea ufafanuzi juu ya  mradi huo Amina majid kutoka Taasisi ya Al-Waleed na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO  Michel Toto Wamesema Tanzania ni miongoni mwa wanufaika wa mradi huo unaofanya vizuri katika Nchi  mbalimbali ikiwemo Nchi za Kiarabu na Agentina.

 

Mradi wa Al-waleed Philanthropies Project unaenda kutekelezwa na shirika la Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO .

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.