Habari za Punde

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Awataka Watumishi wa Hospitali ya Rufaa Bombo Kufanyakazi kwa Bidii

WAZIRI wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwa timu ya usimamizi wa huduma za Afya Mkoa (RHMT) na Timu ya uendeshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo (HMT) mara baada ya kutembelea hospitali hiyo,(kulia kwake) ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo Dkt  Rashid Suleiman akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali hiyo Dkt Joseph Mberesero
KATIBU wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Abasi Mlawa akimueleza jambo wakati wakati wa ziara yake alipozungumza na timu ya hospitali hiyo (HMT)

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) katikati akisisitiza jambo kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Dkt Rashid Suleiman kulia ni Dkt Juma Ramadhani ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Matibabu ya  Dharura katika Hospitali hiyo (EMD) 





Na Oscar Assenga,TANGA


WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo huku akiwataka watumishi wa Hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuhakikisha wagonjwa wanaokwenda wanapata huduma.

Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) amefanya ziara ya kutembelea kwenye hospitali hiyo ambapo pamoja na mambo mengine alizungumza na timu ya hospitali hiyo (HMT) ambapo aliwataka madaktari na wauguzi kuhakikisha wanatoa maelezo sahihi ya wagonjwa wanaolazwa na ndugu.

Amesema hatua hiyo itawaepusha kuwaondolea wagonjwa sintofahamu hususani wanapokuwa wakiulizwa na aina ya ugonjwa anapouluzwa na ndugu zake .

Akiwa kwenye mazungumzo hayo aliwataka watumishi wa Hospitali hiyo kufanya kazi kwa waledi mkubwa hususani katika kuwahudumia wagonjwa wanaofika kupata huduma za matibabu.

Hata hivyo amewapongeza watumishi kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kuwatiaa moyo huku akiwataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.