Habari za Punde

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi akutana naWaziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia, Colombo Sri Lanka


Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Mheshimiwa Suleiman Masoud Makame, leo asubuhi, pembezoni mwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa IORA, unaofanyika Colombo, Sri Lanka, amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia, Ndugu Zambry Abdul Kadir na kuzungumzia masuala mbali mbali ya mashirikiano katika nyanja za uchumi ikiwemo Uchumi wa Buluu, biashara na uwekezaji, nishati, mafuta na gesi, elimu, afya, kilimo na utalii.

Waziri Abdul Kadir amesema kuwa Malaysia ina mpango makhsusi wa kutanua wigo wake wa mashirikiano katika nyanja mbali mbali za uchumi na uwekezaji katika Afrika Mashariki, na hususan Tanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.