Habari za Punde

Ufunguzi wa Kongamano la Kumuenzi Maalimu Seif Hamad Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar

Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla (kushoto) mara alipowasili kwa ajili ya ufunguzi wa kongamano la siku mbili la kumuenzi maalim Seif. Picha na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  mhe. Othman Masoud Othman, akisalimiana na  Bwana Mmusi Maimane (kulia) ambaye ni Kiongozi wa Chama cha upinzani cha Afrika Kusini mara  Mhe. Othman alipowasili katika hoteli ya golden Tulip kiembesamaki kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la siku mbili la kumuenzi marehemu  maalim Seif. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar Mhe. Hemed  Suleiman Abdulla,( kulia)  akisalimiana na Waziri wa Afya wa Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui alipowasili huko hoteli ya Golden Tulip uwanja wa ndege Zanzibar kuhudhuria ufunguzi wa kongamano la siku mbili la kumuenzi marehemu maalim seif (katikati) ni mjane wa marehemu Maalim Seif Mama Awena sinani Masoud. Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa rais  wa Zanzibar .

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  mhe. Othman Masoud Othman, akihutubia kufunua kongamano la siku mbili la kumuenzi marehemu maalim seif sharif amad huko  katika hoteli ya golden Tulip kiembesamaki  Zanzibar leo tarehe 25.11.2023. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.