Habari za Punde

Wizara ya Katiba na Sheria watakiwa kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano

 Baadhi ya watendaji wa wizara ya katiba na sheria  wakifuatilia taarifa ya utekelezaji  wa Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai hadi Septemba iliyotolewa na Waziri   Haroun Ali Suleiman mbele ya   kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa kitaifa ya Baraza la Wawakilishi   
Waziri wa Nchi OR Katiba ,  Sheria ,Utumishi na Utawala Bora akitoa  taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo kwa kipindi cha julai hadi semptemba mbele ya wajumbe wa kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi 

Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi  Machano Othman Said akizungumza na watendaji wa Wizara ya katiba  na sheria   mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majuku katika Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai hadi Semtemba

PICHA NA OFISI YA KATIBA NA SHERIA


Imani Mtumwa  -  Maelezo                                

Wafanya kazi wa Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar wametakiwa  kufanya kazi kwa weledi na Ushirikiano ili  kuwatumikia vyema Watumishi na wananchi ambao wanahitaji kupatiwa huduma kupitia Wizara hiyo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongonzi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Machano Othman Said wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo   kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2023 huko Mazizini.

Amesema umoja na Ushirikiano ndio njia pekee ya kuleta ufanisi katika utendaji kazi na kupelekea upatikanaji wa huduma za Wananchi  kwa haraka zaidi.

Aidha kamati hiyo imewataka Viongozi wa Wizara hiyo kulinda maslahi ya Watumishi wa Umma ili watumishi wafanye kazi kwa bidii na kujituma kwa kutimiza malengo ya Serikali.

Kufuatia Ongezeko la  Talaka Nchini Mwenyekiti huyo  aliitaka Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar na Ofisi ya Wakfu kufanya uchunguzi juu ya suala hilo  na kulipatia ufumbuzi ili kuifanya Jamii kuwa na amani na utulivu .

Kwa upande wake Waziri wa Nchi (OR)Katiba, Sheria,Utumishi  na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman amesema  kwa kipindi cha Julai hadi Septemba Wizara imefanikiwa kusimamia upatikanaji wa haki, kutoa huduma za msaada wa kisheria pamoja na mapitio na marekebisho ya Sheria mbalimbali .

Pia amesema kwa kipindi hicho wamefanikiwa kusimamia uajiri, haki na nidhamu kwa Watumishi , usimamizi wa uendeshaji wa utumishi wa umma  Sambamba na masuali ya Serikali mtandao.

Aidha ameeleza kuwa katika kipindi hicho cha Miezi mitatu ya utekelezaji Wizara vilikabiliwa na  changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa Watumishi wa Tume ya Maadili hasa katika fani na kada za Sharia, uchunguzi, mipango na uchache wa Wafanyakazi wenye fani zinazotakiwa kulingana na mahitaji na muda.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.