Habari za Punde

WAZIRI JAFO ASHIRIKI MKUTANO WA UNEA6 KENYA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akishiriki Mkutano wa Sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA6) unaofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) jijini Nairobi, Kenya ambapo ulifunguliwa Februari 26, 2024 na kutarajiwa kuhitimishwa Machi 01, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo anashiriki Mkutano wa Sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA6) unaofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) jijini Nairobi, Kenya.

Kupitia mkutano huo viongozi kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania wanajadili namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa baionuayi na uchafunzi wa mazingira.

Kama inavyofahamika Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo husababisha ukame, uhaba wa mvua, mafuriko na vifo vya mifugo.

Pamoja na kushiriki Mkutano wa UNEA6, katika kukabiliana na changamoto hizo Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kuhakikisha taifa linakuwa salama.

Lengo la mkutano huo ni kuunda sera kuhusu mazingira ambapo UNEA linalenga kurejesha maelewano kati ya binadamu na mazingira na hivyo kuboresha maisha ya watu wanaokabiliwa na changamoto za mazingira.

Hivyo, mkutano huu ni fursa pia kwa serikali za nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa, wanaharakati wa mazingira, wanasayansi na sekta binafsi kupaza sauti na kuhusishwa katika kutunga sera ya ulimwengu mzima kuhusu mazingira.

Ujumbe wa Tanzania umeambatana na Waziri Dkt. Jafo ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi na wataalamu kutoka Ofisi hiyo.

Mkutano huu wenye kaulimbiu ‘Juhudi madhubuti, jumuishi na endelevu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi‘ ulifunguliwa unatarajiwa kuhitimishwa Machi 01, 2024.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.