Habari za Punde

Wizara ya Utamaduni Kushirikiana na Drums Beat Carnival Tamasha la Utamaduni

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Nicholas Mkapa (kushoto) amesaini Mkataba wa Ushirikiano na Bw. Mwesiga Selestine  ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Drum Beats Carnival Tanzania Limited kuhusu ushirikiano katika uendeshaji wa Tamasha la Kitaifa la  Utamaduni ambalo hufanyika kila mwaka nchini.

Halfla hiyo imefanyika Machi 25, 2024 katika Ofisi za Wizara Mtumba Jijini Dodoma na kushuhudiwa na baadhi ya Viongozi wa Wizara hiyo.

Akizungumza mara baada ya kusaini Mkataba huo, Naibu Katibu Mkuu Mkapa amesema Mkataba huo ni mwanzo mzuri wa kushirikiana na Sekta binafsi katika kuendesha matamasha ya wizara hiyo pia kupanua wigo kwa wadau wa sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika uendeshaji wa matukio ya kijamii.


Kwa upande wake mwakilishi wa Kampuni hiyo Bw. Mwesiga amesema Kampuni hiyo itahakiksha  Tamasha hilo linafanyika kwa ufanisi na kukidhi mahitaji ya wizara katika kutoa furaha kwa watanzania.

Tamasha la tatu la Utamaduni linatarajiwa kufanyika mwezi Agosti, 2024 Mkoani Ruvuma.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.