Habari za Punde

Dua ya Kumuombea Brigedia Jenerali Mstaafu Yussuf Himid Maftaha Kuwaenzi Viongozi Wanamapinduzi Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma akiwa pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika Dua ya kumuombea  Brigedia Jenerali Mstaafu Marehemu Yussuf Himidi Maftah Ikiwa ni katika muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa hafla iliofanyika katika Msikiti wa Sharifu Msa Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja.

Na Sheha Sheha, Maelezo - 03/04/2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma amesema Serikali inathamini mchango wa Viongozi wa Kitaifa katika kuleta maendeleo Nchini.


Ameyasema hayo wakati wa Ziara ya kusoma Dua katika Kaburi la Bregedia Jenerali Mstaafu Marehemu Yussuf Himid Maftah huko Mtoni Wilaya ya Magharibi “A”.

 

Aidha amesema kuwa, Ujasiri na uzalendo wa Viongozi hao ndio uliopelekea kuleta uhuru na maendeleo nchini hivyo Serikali itaendelea kuwaenzi kwa kuendeleza utaratibu uliowekwa wa kumuombea Dua Muasisi huyo.


“Nchi yetu imepitia Vipindi mbalimbali, ikiwemo kipindi cha ukoloni, ujasiri na uzalendo wa Viongozi hawa ndio uliochangia kuleta uhuru Nchini”


Aidha, amewaomba Wananchi kuendeleza utamaduni ulioachwa na Viongozi hao ikiwemo Amani, umoja na upendo kwa mustakbali mwema wa maendeleo Nchini.


Akizungumza kwa Niaba ya familia, Ndg. Abbas Himid Yussuf ameishukuru serikali kwa kuendeleza utaratibu huo wa kuwakumbuka na kuwajali Viongozi hao.


Dua ya kumuombea marehemu brigedia generali mstaafu Yussuf Himid Maftah ni miongoni mwa Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ambapo huanzia tarehe mosi April ya kila mwaka na kilele chake kinatarajiwa kufanyika tarehe 07 April, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma akizungumza na Wananchi na Wanafamilia baada ya kumaliza Dua ya kumuombea  Brigedia Jenerali Mstaafu Marehemu Yussuf Himidi Maftah Ikiwa ni katika muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa hafla iliofanyika katika Msikiti wa Sharifu Msa Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Baadhi ya Wananchi na wanafamilia waliohudhuria katika Dua ya Brigedia Jenerali Mstaafu Marehemu Yussuf Himidi Maftah Ikiwa ni katika muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa hafla iliofanyika katika Msikiti wa Sharifu Msa Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma akimkabidhi Kiongozi wa Familia Abasi Himidi Yussuf Ubani baada ya kumaliza Dua ya kumuombea  Brigedia Jenerali Mstaafu Marehemu Yussuf Himidi Maftah Ikiwa ni katika muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa hafla iliofanyika katika Msikiti wa Sharifu Msa Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Kiongozi wa Familia Abasi Himidi Yussuf akitoa Neno la Shukurani baada ya kumaliza Dua ya kumuombea  Brigedia Jenerali Mstaafu Marehemu Yussuf Himidi Maftah Ikiwa ni katika muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa hafla iliofanyika katika Msikiti wa Sharifu Msa Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.