Habari za Punde

RAIS SAMIA ASHIRIKI MSIBA WA MZEE MUSSA ABDULRAHMAN, UNGUJA ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole na kumfariji Bi. Mwanakheri Mussa Yussuf, Mjane wa Marehemu Mzee Mussa Abdulrahman ambaye alikuwa rafiki wa familia na Jirani wa karibu aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo mtaa wa Mombasa, Zanzibar. Rais Samia alifika kutoa pole msibani Kwahani Mchangamwingi Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji Bi. Mwanakheri Mussa Yussuf, Mjane wa Marehemu Mzee Mussa Abdulrahman ambaye alikuwa rafiki wa familia na Jirani wa karibu aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo mtaa wa Mombasa, Zanzibar, kushoto ni Mtoto wa Marehemu Bi. Fatma Mussa Abdulrahman. Rais Samia alifika kutoa pole msibani Kwahani Mchangamwingi Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiomba dua pamoja na Wanafamilia wa Marehemu Mzee Mussa Abdulrahman aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo mtaa wa Mombasa, Zanzibar. Rais Samia alifika kutoa pole msibani Kwahani Mchangamwingi Zanzibar tarehe 16 Aprili, 2024.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.