Habari za Punde

Polisi Tanzania Kushirikiana na Polisi wa Nchi za Falme za ANchi za Kiarabu

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP.Hamad Khamis Hamad akizungumza na Balozi Mdogo wa Nchi za Falme za Kiarabu anayefanyia kazi zake Zanzibar Mhe.Saleh Ahmed Al Hemeiri mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Kilimani Zanzibar leo 29-4-202.
Balozi Mdogo wa Nchi za Falme za Kiarabu anayefanyika Kazi zake Zanzibar Mhe.Saleh Ahmed Al Hemeiri akimkabidhi zawadi Kamishna wa Jeshi la Polizi Zanzibar CP.Hamad Khamis Hamad, baada ya kumaliza mazungumzo hayo yaliofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar. 

Na.Omar Hassan  na Said Bakar -Polisi  Zanzibar. 29/04/2024

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP.Hamad Khamis Hamad amesema ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Nchi za Falme za Kiarabu kutatoa fursa za kubadilishana uzoefu baina ya pande mbili hizo na kupelekea kuimarika kwa ulinzi katika miradi ya maendeleo nchini. 

Akizungumza na Kamishna wa Polisi Zanzibar CP.Hamad Khamis Hamad amesema ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Nchi za Falme za Kiarabu kutatoa fursa za kubadilishana uzoefu baina ya pande mbili hizo na kupelekea kuimarika kwa ulinzi katika miradi ya maendeleo nchini. 

Nae Balozi Mdogo wa Nchi za Falme za Kiarabu Mhe.Saleh Ahmed Al Hemeiri  amesema ziara yake Makao Makuu ya Polisi Zanzibar ni kuendeleza ushirikiano wa kihistoria baina ya Tanzania na Nchi za Falme za Kiarabu na ameahidi kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi Baina ya Tanzania na UAE.

Aidha amesifu hali ya ulinzi na usalama iliopo Tanzania inayopelekea Raia wa Falme za Kiarabu na Raia wa Nchi nyengine wanaotembelea Zanzibar kufanya kazi zao wakiwa katika hali ya Amani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.