RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Masheikh mbalimbali wa
Zanzibar, wakati wa hafla maalumu iliyoandaliwa na Ofisi ya Mufti Mkuu na
kuzindua Kamati ya Kitaifa ya Kusimamia Madrasa Zanzibar, mazungumzo hayo
yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Mazizini Wilaya
ya Magharibi “B” Unguja 26-6-2025.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waumini wa Dini ya
Kiislamu katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja,
wakati wa hafla ya Kilele cha Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1447 Hijria.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh. Saleh Omar Kaabi, baada ya kumazika kwa Kilele cha Maadhimisho ya Mwaka
Mpya wa Kiislamu 1447 Hijria, iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar
Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja 26-6-2025.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Masheikh mbalimbali wa Zanzibar, baada ya kumazika kwa Kilele cha Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1447 Hijria, iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 26-6-2025.
No comments:
Post a Comment