Habari za Punde

WAZIRI MKUU AZINDUA MITAMBO YA UCHORONGAJI NA VIFAA VYA UTAFITI WA MADIN


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza wa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde aliyetoa maelezo baada ya Waziri Mkuu kuzindua mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini kwa wachimbaji wadogo kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano ha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 24, 2025

Baadhi ya mitambo ya  uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini kwa wachimbaji wadogo ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliizindua kwenye viwanja vya Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 24,2025.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alipozindua mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini kwa wachimbaji wadogo kwenye viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma , Juni 24, 2025. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mteule na IGP Mstaafu, Balozi Simon Sirro
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini kwa wachimbaji wadogo, kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 24, 2025.  Wa tatu kulia ni Waziri wa mdini, Anthony Mavinde, wa tano kulia ni Mkuu wa Mkoa  wa kigoma Mteule, Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la madini la Taifa (STAMICO) na IGP Mstaafu, Balozi Simon Sirro. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati aya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Same Magharibi, Dkt. Mathayo David na wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa VIti Maalum Mstaafu, Lediana Mg’ong’o alipotemblea banda la maonesho la mkaa bora wa Rafiki Briquettes alipozindua mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini kwa wachimbaji wadogo, Juni 24, 2025.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipozindua mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini kwa wachimbaji wadogo kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 24, 2025.

Washiriki wa uzinduzi wa  mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini kwa wachimbaji wadogo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  alipozungumza katika uzinduzi huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 24, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.