Habari za Punde

Waziri Mhe.Tania Azindua Mashindano ya Baskeli yalioshirikisha nchi mbali mbali za Afrika Mashariki pamoja na Dubai yalioandaliwa na Zanzibar International Sports Fertival

Waziri wa Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo akizindua Mashindano ya Baskeli yalioshirikisha nchi mbali mbali za Afrika Mashariki pamoja na Dubai yalioandaliwa na Zanzibar International Sports Fertival  huko Forodhani Wilaya ya Mjini.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema Serikali inaimarisha miundombinu ya michezo ili kuibuwa vipaji na kukuza Utalii.


Hayo ameyasema huko katika Uzinduzi wa mashindano ya mbio za Baskeli yaliyotayarishwa na Zanzibar International Sports Festival yaliofanyika Forodhani,Wilaya ya Mjini .

Amesema Serikali inaendelea kujenga miundombinu ya michezo hivyo kuna kila sababu ya kukaribisha wageni wa Mataifa mbali mbali kushiriki katika mashindano mbali mbali ya michezo

Mheshimiwa Tabia aliwaahidi  kushirikiana nao  kwa kuwapatia huduma nzuri  pamoja na kuwakaribisha maeneo ya kiutalii na maeneo ya kihistoria ili waweze kujifunza historia ya Zanzibar .

Nae Rais wa Chama Cha Baskeli Afrika Gadfrey Jacks Mahagama  amesema wamefarijika kushiriki katika mashindano ya Baskeli hapa Zanzibar jambo ambalo litasaidia kuongeza mashirikiano na udungu uliopo katika nchi za Afrika mashariki .

Amesema kuwa nchi zilizoshiriki katika mashindano hayo Zanzibar ambayo ni wenyeji Tanzania bara ,Kenya ,Uganda, Congo,Dubai, Burundi pamoja na Sudan .

Ameeleza kuwa kufanyika Kwa mashindano hayo ni kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mapinduzi wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Husein Ali Mwinyi pamoja na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita katika Juhudi kubwa ya kuimarisha sekta ya michezo nchini .

Amesema mashindano ya mbio za Baskeli ni ya siku tatu ambayo yamejumuisha  washiriki 150 kutoka nchi mbali mbali mashindano hayo yataanzia Maisara kuelekea Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja, kumalizika Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja  .

Amesema kwamba mbali na mashindano hayo kutakuwepo na mashindano ya Timu za Ufukweni kutoka Zanzibar na wapinzania wao kutoka Kenya .

Mashindano ya mbio za Baskeli Zanzibar (international fastoval sports festival 2025, imejumuisha kiasi ya wanachama 150 kutoka mataifa mbalimbali  iiwemo Burundi, Congo, Uganda, Dubai, Tanznia Bara na wenyeji Zanzibar.











Imetayarishwa na kitengo cha Habari,
WHVUM.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.