Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Amefungua Maonesho ya Wiki ya Ardhi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema katika kuhakikisha matumizi mazuri ya ardhi na makaazi yanafikiwa ni wajibu wa kila mmoja kuwa tayari kuyapanga vizuri maeneo yao ya ardhi na makaazi ili kuweza kuwavutia wawekezaji wakubwa duniani kuja kuekeza visiwani Zanzibar .

Ameyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa maonesho ya wiki ya ardhi na makaazi yanayofanyika katika uwanja wa New Aman Complex Zanzibar.
Amesema Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi inapaswa kuranya majukumu yake kwa uweledi mkubwa na kwa haki ili kutimiza wajibu wa kuwa ba matumizi bora ya ardhi na makaazi yatakayotoa mchang mkubwa katika naendelea ya Zanzibar.

Mhe. Hemed amesema kupitia wiki ya ardhi wananchi watapata fursa mbali mbali ikiwemo kuelewa mchakato wa kumiliki ardhi na makaazi kwa njia halali na sahihi pamoja na kutambua taratibu za kusajili ardhi, kupumwa, upatikanaji wa hati na uhaulishaji wa ardhi.

Aidha, amefahamisha kuwa katika juma hilo la ardhi na makaazi elimu inatolewa kuhusu ujenzi salama, mpangilio wa mji, makaazi rafiki kwa mazingiri pamoja na kujengewa uwelewa juu ya kujiunga na Jumuiya za Makaazi ya pamoja (Kondomino) na faida zake.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametoa wito kwa wanachi na wadau wote wa sekta ya ardhi na makaazi kushirikiana katika kulinada rasilimali ya ardhi na makaazi kwa matumizi endelevu kwa faida ya vizazi vilivyopo sasa na baadae.

Ameiagiza wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kuendelea kuadhimisha wiki ya ardhi ambayo inaweza  kuimarika kwa kiasi kikubwa na kujumuisha wadau wengi zaidi na kuleta tija zaidi.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Rahma Kassim Ali amesema kwa lengo la kudhibiti matumizi mabaya ya ardhi, wizara ya ardhi imeamua kujenga majengo ya kisasa ya ghorofa ambayo huchukua nafasi ndogo ya ardhi inayochukua wakaazi wengi kwa wakati mmoja.

Waziri Rahma meseishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuipatia wizara ya ardhi vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi kwa lengo la kuboresha ufanyaji kazi na utowaji wa huduma bora kwa wananchi.

Amewataka wananchi kushirikiana na wizara ya ardhi kwa kufuata maelekezo na elimu wanayopatiwa juu ya matumizi bora na salama ya ardhi na makaazi makaazi ili kuendelea kulinda ubora na thamani ya ardhi tuliyonayo.

Baadhi ya washiriki wa maonesho hayo kutoka Taasisi mbali mbali za serikali wameelezea kazi wanazozifanya na kwa namna gani watafaudika na maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.