KATIBU wa CCM Wilaya ya Mfenesini, Veronica Ndaro, akimkabidhi Mihayo Juma Nhunga, fomu ya kuwania uwakilishi wa jimbo la Mwera.
KATIBU
wa CCM Wilaya ya Mjini, Bilali Hassan Maulid (kushoto), akikabidhi fomu ya
kuomba uteuzi kugombea Ubunge kupitia
CCM jimbo la Kwahani kwa Mkurugenzi wa Jumuiya ya Kupambana na Changamoto za
Mabadiliko ya Tabianchi Zanzibar (ZACA), Mahfoudh Haji katika ofisi za chama hicho
zilizomo katika jengo la Thabit Kombo Mall Michezani.
KATIBU wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Kusini Unguja, Pili Issa Juma, akimkabidhi
Farida Hamad Seif, fumo ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa Ubunge wa mkoa wa
Kusini kupitia viti maalumu walemevu.
KATIBU
wa Mkoa wa Magharib (UWT), Salama Juma (kulia), akimkabidhi Nafisa Madai fomu
ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa Ubunge wa viti maalum mkoa wa magharibi.
KATIBU wa CCM Wilaya ya Kati Unguja, Omar Justas Moris, akimkabidhi
Mustafa Omar Kibe, fomu ya kuwania uwakilishi jimbo la Tunguu zoezi
lililofanyika ofisi za CCM wilayani humo.
KATIBU wa CCM Wilaya ya Kati Unguja, Omar Justas Moris (kushoto),
akimkabidhi Ali Haidar Madoweya, fomu ya kuwania Ubunge jimbo la Uzini zoezi lililofanyika ofisi za CCM wilayani
humo.
KATIBU wa CCM Wilaya ya Mfenesini, Veronica Ndaro, akimkabidhi Mudrik
Ramadhan Soraga fomu ya kuwania uwakilishi wa jimbo Bububu zoezi lililofanyika katika
ofisi za Bububu.
No comments:
Post a Comment