Habari za Punde

Fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB Kufanyika Uwanja wa New Amaan Complex Kesho Bingwa Mtetezi Yanga Kumenyana na Singida Bis Star.

 Kocha Mkuu wa timu ya Singidar Black Star   David Ouma malengo yao makubwa ni kuhakikisha wanatwaa kombe la shirikisho la CRDB katika mchezo huo utakaofanyika katika uwanja wa new amaan complex Zanzibar.


Na Hawa Abdallah. Zanzibar 

MABINGWA wa Ligi kuu Tanzania bara ambae pia Bingwa metetezi wa Kombe  la shirikisho la benki ya CRDB   Yanga SC wanashuka uwanjani leo kuwavaa Singida Big star katika mchezo wa Fainali wa michuano hiyo.

Mchezo huo wa  Fainali unachezwa katika uwanja wa New Amaan Complex Visiwani hapa  majira saa mbili Usiku.

Akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa habari Kocha mkuu wa yanga SC   Miloud Hamdi alisema mchezo wowote wa fainali ni mchezo mgumu hivyo hawatauchukulia kama mchezo rahisi kwao.

Alisema wanawajua wapinzani wao vizuri kupitia michezo ya Ligi kuu hivyo wamejiandaa kuhakikisha wanatetea taji lao.

Alisema  wekuja kushinda mchezo huo muhimu ambao utakwenda kukamilisha vizuri msimu wao huu wa 2024/2025.

“Ni mchezo muhimu na nimchezo mgumu, lakini mipango yetu ni kuhakikisha tunachukua kombe hili kwa mara nyingine tena”alisema.

Alisema kikosi chake kimejiandaa na  katika kuwakabili wapinzani wao hao na hawatauchukulia mchezo wa kawaida ili kuona lengo lao linatimia kwa asilimia kubwa.

Nae Mchezaji wa timu ya Yanga SC Sheikhan Khamis  alisema kwa kushirikiana na wachezaji wenzake wamejiandaa kufanya vizuri kwa kufuata maelekezo ya mwalimu wao.

“ Tumejiandaa kuahakikisha tunafanya kile ambacho mwalimu wetu ametuelekeza tukifanye, ili kutimiza lengo la kutetea ubingwa huu”alisema.

Nae Kocha Mkuu wa timu ya Singidar Black Star   David Ouma malengo yao makubwa ni kuhakikisha wanatwaa kombe la shirikisho la CRDB katika mchezo wao wa Leo.

Alisema kila timu inakuwa na maono yake mwanzo msimu hivyo  mipango yao ipo kuhakikisha wanafanikiwa mpango huu uliobaki katika michuano hii.

Alisema  Singida Black star ndio timu pekee ambayo ilikuwa na ugumu katika kuitafuta fainali ni lazima kuhakikisha wanamaliza Fainali kwa kuchukua kombe hilo.

“Kama ambavyo tulipambana kuitafuta fainali na tukafanikiwa na ndivyo tutakavyo pambana kunyakuwa kombe hili”alisema.

Fainali ya michuano hiyo ya Kombe la shirikisho la CRDB ni kwa mara ya pili linafanyika hapa Visiwani  Zanzibar katika dimba la New Amaan Compelx.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.