Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Azungumza na Masheikh na Kutowa Mkono wa Eid Fitry kwa Wananchi wa Zanzibar Viwanja vya Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Viongozi wa Dini na Masheikh katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar walipofika kumsalimia na kumtakia Kheri ya Sikukuu ya Eid Fitry, na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utaweala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.
VIONGOZI wa Dini na Masheikh Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akizungumza na Masheikh hao katika ukumbi wav Ikulu Jijini Zanzibar, walipofika kwa ajili ya kumsalimia na kumtakia kheri ya Sikukuu ya Eid Fitry, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 10-4-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Masheikh na Viongozi wa Dini katika kuitikia dua ikisomwa na Sheikh. Khamis Abdulhamid (hayupo pichani) baada ya kumaliza kumsalimia na kumtakia Kheri na Sikukuu ya Eid Fitry, na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Masheikh na Viongozi wa Dini katika kuitikia dua ikisomwa na Sheikh. Khamis Abdulhamid (hayupo pichani) baada ya kumaliza kumsalimia na kumtakia Kheri na Sikukuu ya Eid Fitry, na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Sheikh. Khamis Abdulhamid, baada ya kumaliza kumsalimia na kumtakia Kheri na Sikukuu ya Eid Fitry, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-4-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsalimia na kutowa mkono wa Eid Fitry kwa Mwananchi Bi.Lozi Ali wa Ali, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-4-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi waliofika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kumsalimia na kumtakia Kheri ya Sikukuu ya Eid Fitry, na kutowa mkono wa Eid kwao
WANANCHI waliofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kumsalimia na kumtakia Kheri ya Sikukuu ya Eid Fitry, wakimsikiliza Rais wa Zabzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakati akiwasalimia na kutwapa mkono wa Eid Fitry katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-4-2024

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.