Habari za Punde

Dk.Mwinyi : Ameihakikishia Serikali ya Brazil ushirikiano mzuri uliopo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi mpya wa Brazil Nchini Tanzania Mhe.Gustavo Martins Nogueira alipofika Ikulu Jijini Zanzibarb leo 13-5-2024 kwa ajili ya mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Brazil Nchini Tanzania Mhe. Gustavo Martins Nogueira, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-5-2024, alipofika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na kujitambulisha.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, 

Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameihakikishia Serikali ya 

Brazil ushirikiano mzuri uliopo na Serikali ya Mapinduzi ya 

Zanzibar hasa kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo.                                            

Rais Dk. Mwinyi ameyaeleza hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Balozi mpya wa Brazil nchini Tanzania, Mhe. Gustavo Martins Nogueira na ujumbe wake wake aliofika kujitambulisha.

Katika mazungumzo yao wamegusia kuendeleza uhusiano uliopo baina ya Zanzibar na Brazil kwenye nyanja mbalimbali za miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya Afya, miundombinu ya barabara, ujenzi wa uwanja wa ndege wa Pemba, kuimarisha ushirikiano wa biashara, Utalii pamoja na fursa za uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi Zanzibar.

Kuhusu sekta ya biashara, Rais Dk. Mwinyi alimueleza balozi huyo kwamba Zanzibar haina eneo kubwa kwa kilimo badala yake imejikita zaidi kwenye Sekta ya Utalii na Uchumi wa Buluu pia ni kutuo kikubwa cha biashara kwa watu kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Dk. Mwinyi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanbar itadumisha ushirikiano wake na Brazili hususan kwenye biashara ya sukari na mchele ili kupungumza mfumko wa bei za bidhaa hizo nchini.

Alisema, Zanzibar imejaaliwa baraka ya visiwa vizuri vyenye mvuto vya Unguja na Pemba vyenye ardhi ya uwekezaji, hivyo alimueleza balozi huyo kuangalia fursa ya uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi ambako serikali imeelekeza nguvu zake huko kuvutia wawekezaji kwa eneo hilo.

Akizungumzia Sekta ya Afya Rais Dk. Mwinyi aliemweleza Balozi huyo nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo baina yake na Brazili pia kudumisha na kuendelea kutoa ushirikiano kwa timu ya madaktari wa Brazil wanaokuja Zanzibar kwa nia ya kuendeleza ushirikiano wao kwenye sekta ya Afya hasa kwa sekta ya Afya ya uzazi.

Kwa upande wake, Balozi Nogueira amemueleza Rais Dk. Mwinyi ushirikiano wa pande hizo mbili za diplomasia na kwamba Serikali ya Brazil itaelekeza nguvu zake zaidi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye eneo la afya ya uzazi.

Kuhusu ushirikiano wa biashara Balozi Nogueira pia alimweleza Rais Dk. Mwinyi kwamba Brazili ni msalishaji mkubwa wa Sukari duniani hivyo aliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kushirikiana zaidi kwenye eneo hilo kwa watu wa pande mbili hizo kunufaika na biashara ya Sukari.

Akizungumzia sekta ya Miundombinu ikiwemo ya barabara na mawasiliano Balozi Nogueira pia alimuhakikishia Rais Dk. Mwinyi kuwa Brazil inaendeleza ushirikiano wake na Tanzania hususan Zanzibar kwa kuangalia uwekezaji na kuimarisha uwanja wa ndege wa Pemba ili kutoa fursa zaidi kwa sekta ya Utalii Zanbar kuimarika maradufu.

Uhusiano wa Diplomasia baina ya Tanzania na Brazil ulianza tangu mwaka 1970 na mwaka 1979 Brazili yenye mji mkuu wake Brasilia kwa mara ya kwanza ilifungua ubalozi wake Dar es Salaam,  Tanzania, baadae mwaka 1991 iliufunga kutokana na changamoto za gharama za uendeshaji  lakini mwezi Machi mwaka 2005 Brazili iliufungua tena Ubalozi wake wa Dar es Salaam hadi sasa.

Aidha, Tanzania nayo ilifungua ubalozi wake kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Brasilia mwaka 2007 na mwaka 2010 rais wa kwanza wa Brazil kuitembelea Tanzania alikua Rais wa 39 wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva ambae aliliongoza taifa hilo kutoka mwaka 2003 hadi 2011.

IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Brazil Nchini Tanzania Mhe. Gustavo Martins Nogueira, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-5-2024, alipofika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na kujitambulisha.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Brazil Nchini Tanzania Mhe. Gustavo Martins Nogueira, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-5-2024, alipofika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na kujitambulisha.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Brazil Nchini Tanzania Mhe. Gustavo Martins Nogueira, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-5-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Balozi wa Brazil Nchini Tanzania Mhe. Gustavo Martins Nogueira, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-5-2024.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.