Habari za Punde

Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Azungumza na Waandishi Zanzibar

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ambao utawasili Zanzibar katika Kisiwa cha Pemba tarehe 13 Mei na Unguja Tarehe 17 Mei Ukiwa na kauli mbiu isemayo "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu"hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.

Na.Takdir Ali. Maelezo Zanzibar .10.05.2024.

Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amewaomba viongozi, wafanyakazi, vikosi vya ulinzi na usalama, wananyabiashara, wajasiriamali na wananchi kushiriki katika mapokezi ya mbio za mwenge mwaka 2024.

Mhe. Tabia ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na mapokezi ya mbio za mwenge wa uhuru kwa upande wa Zanzibar.

Amesema mwenge wa uhuru mwaka 2024 kuwasili zanzibar tarehe 13 mai 2024 na kutembezwa katika mikoa na wilaya zote za unguja na Pemba.

Amesema mbio hizo, zinaelimisha na kuhamasisha jamii ya watanzania kuhusu kuzingatia lishe bora, mapambano dhidi ya rushwa, mapambano dhidi ya VVU/ukimwi, dawa za kulevya na ugonjwa wa maleria.

Aidha amesema ujumbe wa mbio za mwenge mwaka huu unalengo la kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi wote wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hususan Tanzania bara  kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa anani na utulivu.

Sambamba na kuendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuhifadhi mazingira kwa ujenzi wa Taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya Maendeleo ya vijana Zanzibar Shaibu Mohd Ibrahim amesema maandalizi ya mbio hizo yamekamilika na miradi mbalimbali kiwemo ya Vijana, Afya na  wajasiriamali inatrajiwa kuzinduliwa katika mbio hizo.

Aidha amesema mwenge wa uhuru upo kwa watu wote na hauna ubaguzi wa rangi, siasa , dini wala kabila hivyo ni vyema wananchi hususan vijana  kujitikeza ili kuweza kufanikisha mbio hizo.

Mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2024, zimezinduliwa rasmi tarehe 02/04/2024 katika kiwanja cha chuo cha ushirikavmoshi mkoani kilimanjaro ambapo mgenirasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Na Ujumbe wa mwenge wa uhuru mwaka huu ni Uhifadhi wa mazingira na uchaguzi wa Serikali za Mitaa chini ya kauli mbiu isemayo tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.