Habari za Punde

Wananchi Kijiji cha Muze Washauriwa Kuweka Akiba Kwenye Vikundi Vilivyosajiliwa

Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha- Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro, akitoa elimu ya fedha kwa Wanavikundi na Wajasiriamali wadogo wadogo katika Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha- Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro (kushoto) akimkabidhi Mjasiriamali Bi. Magreth Kainuka, fulana wakati wa utoaji elimu ya fedha katika Ukumbi wa Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.
Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Bw. Winfred Mwamkalaba (kushoto), akimkabidhi mwanakikundi mjasiriamali Bw. Ruben Masinga, fulana wakati wa utoaji elimu ya Fedha katika Ukumbi wa Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.

Na. Eva Ngowi, WF, Rukwa

Serikali imewataka wananchi kuweka akiba ya fedha zao kwa kuwa akiba ni sehemu mojawapo ya mapato ambayo mwananchi, mfanyabiashara au mjasiriamali anaweza kuhifadhi sehemu salama kwa ajili ya kutimiza malengo aliyojiwekea.

 

Akitoa Elimu kwa Wananchi wa Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini Afisa uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi, Bw. Omar Bakari, alisema ni muhimu kuwa na fedha ya dharura ambayo itasaidia wakati litakapotokea tukio lisilotarajiwa.

 

“Tunaposema tukio la dharura ni kama ajali, misiba, kupoteza kazi, msimu wa njaa na mazingira mengine ambayo hayakutarajiwa.” Alisema Bw. Bakari

 

Bw. Bakari alisema akiba inaweza kuhifadhiwa Benki, Vikundi au SACCOS zilizosajiliwa kwa mujibu wa sheria.

 

Aidha, Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Bw. Winfred Mwamkalaba, alisema kuwa baadhi ya wakazi wa Sumbawanga walizoea kufanya mambo kwa mazoea lakini baada ya huo mfumo wa Huduma Ndogo za Fedha kuanzishwa na kutoa elimu na kuwepo kwa waratibu walioko kwenye halmashauri zingine za mkoa wa Rukwa, imeamsha ari na wengi wanajitokeza kusajili vikundi vyao.

 

“Nitoe wito kwa wananchi wengine ambao wanafanya shughuli zao bila kusajiliwa wafike Ofisi za Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga au wataalamu kutoka kwenye kata ambao wanafanya kazi hizo kwa ajili ya kuwapa miongozo mbalimbali ikiwa ni Pamoja na kusajili vikundi vyao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.