
RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema wakati
umefika wakurejesha diplomasia ya Uchumi na kuendeleza biashara baina ya
Zanzibar na Comoro kwa maslahi ya pande zote mbili.
Dk. Mwinyi ameyasema hayo, Ikulu Zanzibar
alipozungumza na Gavana wa jiji la Moroni, Visiwa vya Ngazija, Bw. Ibrahim Mzee
aliefika na ujumbe wake kuwasilisha dhamira ya kukuza ushirikiano baina nchi
mbili hizo.
Rais Dk. Mwinyi aliushauri ujumbe huo
kurejesha makundi ya wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja Zanzibar kuangalia fursa
za biashara na uwekezaji kama ilivyokuwa miaka iliyopita.
Amesema, ni vyema kwa pande mbili hizo
kufirikia namna ya kurejesha huduma ya usafiri wa vyombo vya baharini ili kuwanufaisha
wananchi wa pande mbili hizo na fursa za biasahara na kijamii ziliopo.
Aidha, Dk. Mwinyi alishauri ujumbe huo
kuweka utaratibu maalumu kwa walimu wa Zanzibar kwenda Comoro kufundisha
Kiswahili au Wakomoro kuja Zanzibar kujifunza lugha hiyo jambo ambalo alisema
litakuwa na wepesi kwani lugha za nchini mbili hizi zinashabihiana.
Naye, Gavana Ibrahimu Mzee amesifu kasi
ya mabadiliko na maendeleo makubwa ya Zanzibar na kusema kuwa nchi yake inakitu
cha kujinza kama ilivyofanikiwa ya Zanzibar.
Alitumia fursa hiyo, kumualika Rais Dk.
Mwinyi kuzuru visiwa vya Ngazija kwalengo la kubadilishana uzoefu kwenye nyanja
za maendeleo.
Eneo jengine alililoligusia ni kuimarisha ushirikiano wa karibu
baina ya Jumuiya ya Wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda (Chamber of
commerce) ya Zanzibar na ile Comoro ili kukuza biashara.
Akiambatana na ujumbe huo Meya wa jiji la Zanzibar, Mahmoud Muhammed
Mussa ameelezea ujumbe wa Gavana huo utakuwepo Zanzibar kwa siku tatu na
kueleza kuwa na mazungumzo ya ushirikiano baina ya Manispaa ya jiji la Zanzibar
na Manispaa ya jiji la Moroni.
Aidha, ujumbe huo utakuwa na siku maalum ya kuutembelea mji
Mkongwe wa Zanzibar ambao mji wa urithi uanaotambulika na UNESCO. Pia ujumbe
huo utafanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa
kwa lengo la kukuza ushirikiano.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment