Habari za Punde

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAISLAMU WA SHIA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwenye Mkutano Mkuu na Kongamano la Umuhimu wa Amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 10, 2024 jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Kongamano hilo lililoratibiwa na Jumuiya ya Waislamu wa SHIA Tanzania, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa vitakavyoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kuwa vinara katika kulinda amani na kukemea viashiria vyote vya uvunjifu wa amani.

Hamasisheni wanachama wenu kushiriki katika uchaguzi huo huku wakizingatia kudumisha amani iliyopo. Wananchi wote waliojiandikisha katika orodha ya wapigakura wa Uchaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wajitokeze kwa wingi kupiga kura katika vituo vyao siku ya Jumatano tarehe 27 Novemba, 2024. Siku hiyo itakuwa ya mapumziko maalum kwa ajili ya uchaguzi huo.”

Ametoa wito huo leo (Jumapili, Novemba 10, 2024) wakati alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Mkuu na Kongamano la Umuhimu wa Amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, jijini Dar es Salaam. “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amewasihi Watanzania na viongozi wa dini kuendelea kuitangaza amani ndani na nje.”

Katika Kongamano hilo, ambalo linaratibiwa na Jumuiya ya Waislamu wa madhehebu ya Shia Tanzania, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwasisitiza viongozi hao kuhamasisha wanachama wao kushiriki katika uchaguzi huo huku wakizingatia suala la kudumisha amani kwa muhimu mkubwa.

Mheshimiwa Majaliwa amesisitiza kwamba kila Mtanzania mwenye sifa ajitokeze kupiga kura ili  kuwachagua vongozi ambao ni mwenyekiti wa kijiji, mwenyekiti wa mtaa, mwenyekiti wa kitongoji na wajumbe wa serikali za vijiji na kamati za mitaa. “Ikumbukwe kuwa kupiga kura ni wajibu na haki ya Kikatiba ya kila  Mtanzania.”

Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali inatambua, inaheshimu na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na madhehebu ya dini pamoja na taasisi zote, ambapo licha ya kutoa mafundisho ya kiroho, taasisi za dini zimekuwa zikiunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali katika kutoa huduma za kijamii kwa wananchi.

Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Alhad Mussa Salum ameipongeza Jumuiya ya Waislam wa Shia Tanzania kwa harakati zake za kuhakikisha amani na utulivu wa Tanzania unaendelea kukua. Mimi ni shuhuda mzuri wa harakati za Shia wanazofanya ili kuhakikisha amani na usalama wa Tanzania unaendelea kuimarika

Viongozi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati  alipozungumza kwenye Mkutano Mkuu na Kongamano la Umuhimu wa Amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 10, 2024 jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Kongamano hilo lililoratibiwa na Jumuiya ya Waislamu wa SHIA Tanzania, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. 
Viongozi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati  alipozungumza kwenye Mkutano Mkuu na Kongamano la Umuhimu wa Amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 10, 2024 jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Kongamano hilo lililoratibiwa na Jumuiya ya Waislamu wa SHIA Tanzania, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu na Kongamano la Umuhimu wa Amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Ramadhan Mwelekwa, Novemba 10, 2024 jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Kongamano hilo lililoratibiwa na Jumuiya ya Waislamu wa SHIA Tanzania, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.