Na.Ali Issa- Maelezo .
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Saada Mkuya Salum amesema Zanzibar kwa mara ya kwanza imepata mkopo wa kibiashara karibu Euro Milioni 400 ambazo zitatumika kwa ajili ya miradi mbali mbali ya Serikali.
Akitaja baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Pemba,Barabara ya Tunguu Makunduchi,barabara ya Chake Chake hadi Mkoani pamoja na Kisauni hadi Fumba.
Hayo ameyasema leo huko Mnazi mmoja katika Ukumbi wa ZBC wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Dkt. Mwinyi katika Wizara ya Fedha na Mipango .
Amesema mkopo huo umepatikana kwa jitihada za Dk. Mwinyi jambo ambalo italeta maendeleo makubwa kwa Zanzibar .
Aidha amesema katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Dk Mwinyi pato la taifa limeongezeka kufikia trilioni 3 na bilioni 758 kutoka trilioni 3 na bilioni 116 ya mwaka 2020 ambayo hiyo inatokana na thamani ya bidhaa pamoja na huduma zinazo zalishwa nchini.
Hata hivyo alisema kuwa Uchumi wa Zanzibar umekuwa hivi sasa kufikia asilimia 7.4 kutoka 1.3 katika mwaka 2020.
“Tumetoka kwenye asilimia 1.3 hadi kufikia asilimia 7.4 hii ni kutokana na jitihada mbalimbali za kujikita katika mifumo hali iliopelekea Uchumi wa nchi kukuwa.” alielezea Mhe. Saada .
Hata hivyo amesema katika mafanikio hayo zaidi ya nyumba 3000 za bei nafuu zitajengwa katika eneo la chumbuni ili kuwawezesha wananchi kupata makaazi ubora kwa bei nafuu.
No comments:
Post a Comment