Katika maongezi na Tume hiyo
iliyoongozwa na Mwenyekiti
wake, Balozi Ombeni Sefue na ujumbe wake, Rais Dk. Mwinyi wamejadili mambo
mbalimbali ikiwemo mapendekezo yatakayo zishauri Serikali mbili za SMZ na SMT
kuhusu masuala ya kodi.
Aidha, Rais Dk.
Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu
Hassan kwa kuiteua Tume hiyo na kueleza kuwa itasaidia kuimarisha na
kubadilisha mifumo ya kodi kwa Serikali zote mbili za SMZ na SMT, itakayoleta
mageuzi kwenye biashara likiwemo eneo la kodi hadi kukamilika kwake.
Kwa upande wake
Balozi Sefue amezishukuru Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya
Mapinduzi ya Zanzibar na kuahidi ushirikiano na Tume hiyo.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment