Viongozi wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni (BASSFU) wameombwa kushirikiana na Wananchi katika kulinda na kutunza Mila, Khulka, Silka, Tamaduni sambamba na Maadili ya kizanzibar.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis (Chilo) ametoa maombi hayo wakati wa Usiku wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni, uliofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakili Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Amesema Dunia ipo katika wakati wa maendeleo ya Sayansi na Teknolojia hivyo ni lazima kulindwa Maadili, Silka na Tamaduni za Nchi sambamba na kuelimisha Vijana ili kuweza kurithisha kizazi cha sasa na baadae.
Aidha amewataka Wasanii kutmia Sanaa zao kwa kuyasemea mambo mazuri yanayofanywa na Marais wa Serikali zote mbili za
Tanzania katika kuwaletea maendeleo Wananchi wao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ndg. Fatma Hamad Rajab amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuimarisha Uchumi wa Zanzibar kupitia sekta mbalimbali ikiwemo ya Sanaa na Utamaduni.
Hivyo amewaomba Wananchi ikiwemo Wasanii kutumia nafasi zao kwa kumuunga mkono Rais wa Zanzibar Mhe. Hussein Ali Mwinyi ili aweze kutekeleza kwa vitendo malengo ya Serikali, kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.
Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya filamu na Utamaduni (BASSFU) na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bi Safia Ali Rijal wamesema kwa kipindi cha miaka 41 ya kuanzishwa BASSFU maendeleo ya Sanaa yamepatikana ikilinganiswa na hapo awali.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis (Chilo) wakati akizungumza katika usiku wa Sanaa, uliokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar huko Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil, Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis (Chilo) akimkabidhi Tunzo màalum, Mtunzi wa Music wa Taarab Prof. Mohammedh l. Nadradin katika Usiku wa Sanaa, uliokwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil, Kikwajuni Zanzibar.
No comments:
Post a Comment