RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Waumini wa Dini ya Kiislam, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa, iliyofanyika leo 6-12-2024 katika Masjid Shaafiy Mbuyu Mnene Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameisistiza jamii kuendelea kuitunza Amani iliopo wakati nchi ikielekea kwenye mwaka wa Uchaguzi Mkuu.
Alhaji Dk. Mwinyi ametoa tamko hilo alipozungumza na Waumini wa dini ya Kiislamu wa kwenye ibada ya sala ya Ijumaa, Masjid Shaafy uliopo Mombasa Mbuyu Mnene, Wilaya ya Magharibi B.
Ameeleza ni wajibu wa Viongozi wa Dini na Wanasiasa kuwahubiria Amani waumini na wafuasi wao ili nchi iendelee kuwa na Utulivu na Serikali iendelee na mipango ya Maendeleo.
Alhaji Dk. Mwinyi amefahamisha kwa miaka minne nchi imekuwa na utulivu mkubwa wa kupigiwa mfano hali inayohitaji kuendelezwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Ameeleza kuwa kwa miaka mingi iliopita Uchaguzi ulikuwa ni sababu ya nchi kuingia katika mifarakano isio na tija kwa Nchi.
Amesisitiza ni vyema kila mwananchi kuwa na dhamira ya dhati ya kuimarisha Amani ili nchi isiingie katika Uhasama na kutokuelewana.
Khatibu wa Masjid Shaafy Khamis Shaaban amewakumbusha Waumini wa Dini ya Kiislamu kuwa na Subira na Ustahamilivu pamoja na kumcha Mwenyezi Mungu kila Wanapopatwa na mitihani ya Kidunia.
Ameeleza kuwa dunia ina mitihani na majaribu mengi na kuwahimiza kumrudia Mungu kwa Sala na Kumshukuru ili kupata shufaa.
Kwanupande wake Katibu wa Afisi ya Mufti, Sheikh Khalid Ali Mfaume amewanasihi Waumini hao kufahamu kuwa Dunia ni pahala pa kutenda mambo mema na kuwa na subira kwani malipo ya wanaosubiri ni pepo.
Wakati huo huo Alhaj Dk,Hussein Ali Mwinyi alifika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Lumumba kuwafariji na kuwajulia hali Wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo akiwemo Mzee wa Chama cha Mapinduzi Haji Machano .
No comments:
Post a Comment