RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya Pamoja na wageni wake Ujumbe wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 7-12-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar inadhamiria kuwa na umeme wa
uhakika kutokana na kutanuka kwa shughuli za uchumi, miradi mikubwa ya
maendeleo, ongozeko la hoteli za kitalii na kasi ya uwekezaji inayokuwa kila
siku.
Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu – Zanzibar
alipozungumza na Ujumbe kutoka Kamisheni ya Umoja wa Ulaya ukiongozwa na Bi.
Rita Laraujinha Mkurugenzi Mwendeshaji wa masuala ya nje, Kanda ya Afrika
waliomtembelea.
Rais Dk. Mwinyi ameeleza kwa muda mrefu Zanzibar imekua ikipokea megawatt 100 za umeme kutoka Tanzania Bara
kupitia waya za chini ya bahari ambao kwa sasa hautoshelezi, hivyo kuna kila
sababu ya kupata umeme mbadala na kufikiria kuwa na umeme wa jua, mawimbi au
upepo, hivyo ameuomba Umoja wa Ulaya (EU)kuangalia uwezekano wa kuisadia
Zanzibar kwenye eneo hilo.
Aidha, alisema,
Serikali inafikiria kuzisarifu taka kwaajili ya kupata umeme mbadala hatua
aliyoielezea mbali yakupata nishati hiyo lakini pia itadhibiditi taka kwani
kumekua na changamoto kubwa ya usimamizi wa taka zinazozalishwa kila siku.
Akizungumzia
uwezeshaji wanawake kiuchumi Dk. Mwinyi ameeleza nia ya Serikali kuwaongezea
nguvu, uwezo na utaalamu kwa wakulima wa mwani ambao asilimia 90 ni wanawake, kwa
kuliinua zao hilo pamoja na kuanzisha viwanda vidogovidogo na vya kati ili
kuusarifu na kuzalisha bidhaa zinazotokana na zao hilo kwa kuziongezea thamani
badala ya kuuza mwani kama malighafi.
Rais Dk. Mwinyi ameusisitiza Umoja wa Ulaya
kuiungamkono Zanzibar katika azma yake ya kukuza Uchumi kupitia sekta za
kimkakati ikiwemo Uchumi wa Buluu na Utalii ambazo ni Sekta za kipaumbele kwa
Serikali anayoiongoza.
Amebainisha kuwa kwa sasa Zanzibar inafanya
utalii wa kisasa unaoshajihisha utalii wa kumbi za mikutano, utalii michezo na
wa afya ambapo awali ilijikita zaidi kuendesha utalii wa fukwe na maeneo ya
urithi ambao umezoeleka kwa muda mrefu.
Akizungumzia masuala ya uwekezaji
amezikaribisha nchi za Umoja wa Ulaya, hususan sekta binafsi kuja Zanzibar
kubaini fursa za uwekezaji ziliopo kwani kuna maeneo mengi hayajafikiwa hasa
kwa sekta ya Uchumi wa Buluu kupitia Utalii, Bandari, Mafuta na gesi pamoja na
sekta ya usafirishaji wa majini.
Pia, Dk. Mwinyi amegusia masuala ya jinsia na
kueleza kuwa Serikali anayoiongoza inafanya kila juhudi kuhakikisha inaweka
uwiano sawa kwa wananwake na wanaume kwa nyanja zote za Elimu, Uchumi, siasa na
ustawi wa jamii na kuuomba Umoja wa Ulaya kuja kuungamkono kwenye maeneo ya
taaluma, kuwajengea uwezo wanawake kwa dhamira ya kuwainua kiuchumi.
Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi ameushukuru Umoja
wa Ulaya kwa ushirikiano uliopo baina yao na misaada wanayoita kwa Tanzania
hususani Zanzibar kwa sekta za jamii hasa kwa Elimu, Afya na Ustawi wa Jamii na
kuwaomba kuendeleza misaada hiyo.
Naye, Bi. Rita Laraujinha ameipongeza Zanzibar
kwa ushirikiano wanaoutoa kwenye Miradi inayosimamiwa na EU na kumuhakikishia
Rais Dk. Mwinyi kuwa wataendelea kuiunga mkono Zanzibar wa kuleta maendeleo
hasa kwa masuala ya afya, elimu na Uchumi wa Buluu.
Amesema, EU imerishwa na hali ya amani na
utulivu uliopo Zanzibar na kwamba Umoja huo utaendelea wakati wote kuunga mkono
juhudi za kuimarisha amani hiyo na kuona Demekrasia inafuata mkondo wake
kwaajili ya maendeleo ya nchi jamii kwa ujumla.
IDARA YA
MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment