Habari za Punde

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- SWALA- MKWAJUNI -KASKAZINI UNGUJA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na waumini wa Masjid ISTIQAMA uliopo Mkwajuni Njia ya Matemwe  Mkoa wa Kaskazini Unguja mara baada ya kumaliza Ibada ya sala ya Ijumaa.

Waumini wa Dini ya Kiislamuna wananchi kwa ujumla wametakiwa kuendelea kuudumisha Umoja na mshikamano uliopo nchini ili kuweza kuisaidia serikali katika kupiga hatua kimaendeleo.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid Istiqama uliopo Mkwajuni njia ya Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja mara baada ya kumaliza  Ibada ya Swala ya Ijumaa.

Amesema eneo lolote lile duniani ili liwe na maendeleo ni lazima wananchi wake wawe na umoja na mshikamano katika harakati zote za kiuchumi na kijamii ili kutiza nalengo ya luwa na Taifa lenye maendeleo endelevu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ni wajibu wa wazazi na walezi kuendeleza utamaduni wa kulea watoto wao malezi ya pamoja yenye kufuata maadili, mila na silka za kizanzibari ambayo yatasaidia katika kupambana na vitendo viovu ikiwemo masuala ya udhalilishaji na madawa ya kulevya ambayo ni janga makubwa linaloiathiri jamii kwa sasa.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewasisitiza viongozi wa dini na wanasiasa kuhakikisha kila wanapokutana na wananchi wanahubiri umuhimu wa kuitunza na kuilinda amani iliyopo nchini inayotoa firsa kwa Serikali kuendelea kuwaletea wanachi maendeleo na jamii kufanya harakati zao za kimaisha kwa utulivu.

Akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Ustadh Juma Ussi Khamis amewataka  waumini wa Dini ya Kiislam kuzidisha ibada hasa katika mwezi huu wa Raajabu ili kuweza kupata fadhila za mwezi huu pamoja na kujiandaa na mwezi mtukufu wa Shaaban na Ramadhan.

Amesema kuwa mwezi wa Raajab ni miongoni mwa miezi Minne ( 4 ) bora katika mwaka hivyo amewasisitiza waumini kuzidisha Ibada pamoja na kuwahimiza watoto wao katika mambo mema ili kuweza kupata wanazuoni wakubwa pamoja na viongozi wenye kufanya haki katika kuongoza kwao.

 

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

Leo tarehe..24. 01. 2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.