Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA CHAMA CHA WAFAMASIA TANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kwaajili ya kufungua Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania leo tarehe 04 Juni 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD) Mfamasia. Mavere Tukai wakati akikagua mabanda mbalimbali ya maonesho katika Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 04 Juni 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Msajili wa Baraza la Famasi Tanzania Bw. Boniface Magige kuhusu usimamizi wa maadili kwa wafamasia nchini wakati akikagua mabanda mbalimbali ya maonesho katika Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 04 Juni 2025.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda pamoja na Viongozi mbalimbali, wakielekea katika Ukumbi Maalum wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 04 Juni 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 04 Juni 2025.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa tuzo kutoka kwa Chama cha Wafamasia Tanzania mara baada ya  Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) leo tarehe 04 Juni 2025. (anayekabidhi tuzo ni Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania Fadhil Hezekiah)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa tuzo iliyotolewa na Chama cha Wafamasia Tanzania kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na maboresho katika sekta ya Afya. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wafamasia Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) leo tarehe 04 Juni 2025. (wanaokabidhi tuzo ni Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe na  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda)











 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.