Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, bi Fatma Hamad Rajab ametia Saini Hati ya
Makubaliano (MOU) na Kampuni Haryana State Electronics
Development Corporation (Hartron) ya Nchini India, kwa
ajili ya kuwasaidia Vijana wa Zanzibar kupata mafunzo na
vifaa, makubaliano ambayo yamefanyika huko Ukumbi wa
Wizara hiyo, Migombani Mjini.
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar
imetiliana saini hati ya Makubaliano (MOU) na Kampuni ya
Haryana State
Electronics Development Corporation (Hartron) ya
Maryana Nchini India kwa ajili ajili ya kuendeleza Vijana wa
Zanzibar.
Utiaji Saini huo, umefanywa na Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imetiwa saini na
Katibu Mkuu wake bi Fatma Hamad Rajab na kwa upande wa
Kampuni ya Harton, imetiwa saini na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni hiyo Dk. Ganesan Jagadesan.
Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo walihudhuria na Balozi wa India
Nchini na Ujumbe wake ambao ulifanyika katika Ukumbi wa
Wizara hiyo Migombani Wilaya ya Mjini.
Akizungumza katika Utiaji Saini wa Makubaliano hayo, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo
Fatma Hamad Rajab amesema lengo ni kusaidia Vijana,
kupata mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(ICT) na Vifaa mbalimbali.
Aidha amesema hali hiyo itatoa fursa mbalimbali kwa vijana
ikiwemo kuwaunganisha pamoja, kupata ajira na kuweza
kufanya kazi kwa Ufanisi.
Kwa uapande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni
ya Haryana State Electronics Development
Corporation kutoka India Dk. Ganesan
Jagadesan ameahidi kufuata maelekezo yalimo katika
Mkataba huo wa Maridhiano ili kuwasaidia Vijana wa
Zanzibar.
Imetolewa na Kitengo cha Habari, WHVUM.
No comments:
Post a Comment