Habari za Punde

 Na.Mwandishi Afya Zanzibar

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema imejipanga katika kukabiliana na magonjwa mbali mbali kwa wananchi, wageni na wanamichezo watakaoshiriki katika mashindano ya CHAN yanayotarajiwa kufanyika mapema mwezi uajao katika visiwa vya Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara maalumu katika Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi Lumumba ambayo ni miongoni mwa Hospitali itakayotumika kutoa huduma wakati wa mashindano ya CAHAN, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amesema Wizara ya Afya Zanzibar imejipanga katika kuahakikisha kuwa usalama wa kiafya kwa wageni na wenyeji  katika mashidano hayo yanakuwa na ubora wa hali ya juu.

Amesema ni fursa ya kipekee kwa nchi ya Zanzibar kuwa mwenyeji wa mashindano hayo na kufanikisha kwa maendeleo makubwa yanaletwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika suala zima la kuimarisha michezo hapa nchini.

Amefahamisha kuwa katika kukabiliana na hali ya kiafya katika kipindi chote cha mashindano ya CHAN Wizara ya Afya imejipanga kwa kuwa na Madaktari wa kutosha, vifaa tiba, usafiri wa dharura pamoja na dawa zote muhimu katika Hospitali ya Lumumba.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Mngereza Mzee Miraji amesema lengo la ziara hiyo ni kuangalia maandalizi ya afya katika kipindi chote cha mashindano ya CHAN yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni hapa nchini.

Aidha amesema   katika kufanikisha mashindano hayo Wizara ya Afya imeandaa mikakati madhubuti ya kuhakikisha wageni na wenyeji na wanamichezo wanakuwa salama na magonjwa na mashindano hayo yanafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Afisa tabibu Mkuu wa Hospitali ya Lumumba Dkt, Yasser El Bahy, amesema Hospitali hiyo ipo tayari kutoa huduma wakati wote kwa wageni na wananchi na kusisitiza kuwa vifaa, Dawa zipo za kutosha katika kukabiliana na hali yoyote.

Ziara hiyo imewashirikisha kamati ya Afya ya CHAN kutoka Wizara ya Afya na imehusisha maeneo tofauti ikiwemo, Hoteli za Kulaza wageni, uwanja wa New Amani Complex, Hospitali ya Mkoa Lumumba ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa  maandalizi ya kiafya yanakwenda sambamba na viwango vinavyohitajika katika mashindano hayo.

Katika hatua nyengine Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh ameitaka kamati ya afya inayoshughulikia maandalizi ya CHAN kukabilina na changamoto na kuimarisha mipango na utekelezaji majukumu yao.

Ameyaeleza hayo katika kikao maalum kwa wanakamati wa afya huko Wizara ya Afya ambacho kimelenga hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya afya kwa ajili mashindano ya CHAN pamoja na kujadili namna kuongeza nguvu katika maeneo yenye changamoto ili kuyaimarisha zaidi.

Mwisho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.