Habari za Punde

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekua na mchango mkubwa kwenye utekelezaji wa masuala ya haki za Binadamu.

Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Wakili Jane Lyimo, amesema Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekua na mchango mkubwa kwenye utekelezaji wa masuala ya haki za Binadamu.

Wakili Lyimo, ameyasema hayo, viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, alipotembelea banda la THBUB katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea viwanjani hapo.

Amesema, wananchi walio wengi wamefanikiwa kupeleka malalamiko yao kwenye tume hiyo pamoja na kukiri kwamba THBUB imekua msaada mkubwa katika kuwapatia ufumbuzi wa  masuala yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.