Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akipokea tuzo maalum ya shukrani kutoka kwa Rais wa TUCTA, Bw. Tumaini
Nyamhokya kwa kutambua mchango wake katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi
nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA)
Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025. Viongozi hao wamempongeza
na kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa utekelezaji wa ahadi yake ya nyongeza ya
mishahara, kupanda madaraja ya watumishi
wa umma na kuboresha mazingira ya kazi nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
Tanzania (TUCTA), Bw. Tumaini Nyamhokya, na ujumbe wake Pamoja na Viongozi wengine wa Serikali, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti,
2025.
No comments:
Post a Comment