Habari za Punde

Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) wamshukuru Rais Dkt. Samia kwa kutekeleza ahadi ya nyongeza ya mishahara ya Watumishi wa Umma

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea tuzo maalum ya shukrani kutoka kwa Rais wa TUCTA, Bw. Tumaini Nyamhokya kwa kutambua mchango wake katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025. Viongozi hao wamempongeza na kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa utekelezaji wa ahadi yake ya nyongeza ya mishahara, kupanda madaraja  ya watumishi wa umma na kuboresha mazingira ya kazi nchini.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Bw. Tumaini Nyamhokya, na ujumbe wake Pamoja na Viongozi wengine wa Serikali, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.