6/recent/ticker-posts

POLISI JAMII YAANZA KUKUBALIKA KUSINI PEMBA

Na Mwanajuma Abdi

MARIDHIANO ya kisiasa yaliyofikiwa nchini yamesaidia kuimarisha zaidi Polisi Jamii katika Mkoa wa Kusini Pemba.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Hassan Nasir wakati akizungumza kwa njia ya siu na gazeti hili mwishoni mwa wiki.

Alisema maridhiano ya vyama viwili vya siasa cha CCM na CUF yamesaidia kutekelezwa vizuri dhana ya Polisi Jamii kwa wananchi wa Mkoa huo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Alieleza kwamba Polisi jamii imeimarika katika Mkoa huo, jambo ambalo limesaidia kupunguza makosa mbali mbali yakiwemo ya jinai.

Kamanda Nasir aliongeza kusema kwamba, wizi wa mazao na mifugo umepungua kwa kiasi kikubwa, ambapo mara nyingi huibiwa ndizi moja ama mbili katika mashamba ya wakulima.

Hata hivyo, alifahamisha kuwa, suala la wizi wa mifugo lililokuwa likiiyumbisha jamii mkoni humo sasa limepungua na badala yake wizi unaojitokeza ni wa kawaida ambao unafanyika katika maeneo mengi. Hata hivyo alifafanua kuwa jeshi hilo litaendelea kupmbana na wizi kwa kuwa hakuna wizi mdogo.

Alifafnua kwamba mafanikio hayo yanatokana na kukubalika kwa mpango kamili wa polisi jamii ambapo kabla ya maridhoiano hayo jambo hilo halikuwa rahisi kufikiwa.

"Hivi sasa wananchi wameungana zaidi kutokana na maridhiano yaliopo, hali hiyo inatokana kukuzwa kwa masuala ya Polisi jamii kwa kuwashirikisha wananchi wenyewe moja kwa moja.

Aidha akizungumzia dawa za kulevya, alisema bado poilisi haijawakamata waingizaji wa dawa hizo lakini wamewakamata vijana 12 ambao waliwapeleka kuchunguzwa (kupimwa) haja ndogo (mkojo) na kubainika kuwa wanatumia.

Alieleza vijana hao wote waliwafikisha mahakamani, ambao ni wakaazi wa Msingini, Miembeni na Mtoni katika Wilaya ya Chake Chake.

Aidha, alifafanua kuwa, katika Mkoa huo hakuna vijana wengi wanaojihusisha na matumizi hayo, ambapo wengine wanaowatilia mashaka walipokwenda kuwapima wanaonekana hawatumii dawa hizo

Post a Comment

0 Comments