Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM,ambae pia ni mlezi CCM Mkoa wa Mjini Magharibi,Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi,wakati wa maadhimisho ya kilele cha kutimiza miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM,sherehe za maadhimisho hayo zilifanyika kwa matembezi ya mshikamano aliyoyaongoza kuanzia uwanja wa Amaan, na hatimae kuzungumza na wanachama katika viwanja vya kisonge Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM,ambae pia ni mlezi CCM Mkoa wa Mjini Magharibi,Dk Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akiongoza matembezi ya mshikamano ya sherehe za kilele za kutimiza miaka 34 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi ,yaliyoanzia Uwanja wa Amaan hadi Viwanja vya Kisonge Mjini Zanzibar jana.Baadhi ya wapenzi na wanachama wa chama cha Mapinduzi wakiwa katika matembezi ya mshikamano ya kusherehekea kutimia miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM yakiongoza na Rais wa Zanzibar,(hayupo pichani)yakielekea viwanja vya Kisonge Mjini Zanzibar jana
Picha na Ramadhan Othman Ikulu
0 Comments