6/recent/ticker-posts

MASHINDANO YA VIJANA A/MASHARIKI 'OLIMPAFRIKA' KUANZA RWANDA

Na Suleiman Bangaya

MASHINDANO ya michezo mbalimbali kwa timu za vijana wa Afrika Mashariki 'Olimpafrika', yanatarajiwa kuanza Novemba 25 hadi 28, nchini Rwanda.

Katika michuano hiyo, Tanzania ambayo ni bingwa wa mpira wa miguu kwa vijana walio chini ya miaka 17, itashiriki mashindano hayo ikiwakilishwa na timu yake iliyoko katika kituo cha vijana huko Dole Wilaya ya Magharibi Unguja.


Ubingwa wa mchezo hao kwa vijana walio chini ya miaka 13, ni Rwanda ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo.

Timu hizo zilitwaa ubingwa huo katika mashindamo yaliyofanyika mwaka jana nchini Burundi.
Mbali na Tanzania na Rwanda, timu nyengine zitakazochuana katika ngarambe hizo, ni Kenya, Uganda, Burundi, pamoja na waalikwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Jumla ya wachezaji 24 na viongozi watatu, waliondoka Zanzibar jana kwa boti hadi Dar es Salaam, ambako walitarajiwa kulala na kuondoka leo kwenda Kigali, Rwanda tayari kwa patashika hiyo.

Wachezaji hao ni Abdulkadir Mgeni, Hassan Mussa, Ramadhan Robert, Nassir Ali, Zakaria Suleiman Almas, Sudi Juma, Steven Wilson, Abbas Mohammed, Farid Suleiman, Iddi Omar, Nassor Ali, na Ramadhan Khamis.

Post a Comment

0 Comments