6/recent/ticker-posts

MEJA SANANDI ATAKA MSHIKAMANO KWA WAPIGANAJI JKU

Na Said Abdul-rahman, Pemba

MKUU wa Kambi ya Ofisi kuu JKU Pemba, Meja Veronika Saimon Sanandi, amewataka wapiganaji wa kambi hiyo kushirikiana kikamilifu katika kutekeleza wajibu wa kazi zao ndani ya jeshi hilo.

Meja Sanandi aliyasema hayo huko katika ukumbi wa ofisi kuu JKU Wawi, wakati wa tafrija ya kuwavisha vyeo wapiganaji wa jeshi hilo ambao wamepanda vyeo ngazi tofauti.


Veronika, aliwataka wapiganaji hao kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza wajibu wa jeshi hilo ili kuliendeleza mbele kimaendeleo, pamoja na kukabiliana na changamoto ambazo zinalikabili jeshi hilo.

“Mliopanda vyeo leo msione kuwa nyinyi ndio mahodari wa kazi bali ni maamuzi ya jeshi lenu kuwateueni nyinyi ili muweze kuwasaidia kazi wakuu wenu”,alisema Meja Vero.

Sambamba na hayo pia Mkuu huyo aliwasisitiza wapiganaji hao kufuata sheria za kazi na kuwacha majungu katika sehemu zao za kazi na kuepukana na tabia ya utoro ambayo itaweza kurudisha nyuma maendeleo
ya jeshi hilo.

Akitoa shukurani zake kwa Mkuu huyo Ofisa mteule daraja la kwanza (Wo1) Khamis Nassor, kwa niaba ya wenzake alimuhakikishia mkuu huyo kuwa watakuwa bega kwa bega na wakuu wao na kushirikiana nao katika kupeleka mbele maendeleo ya jeshi hilo.

Aidha mteule huyo alitoa ahadi kwa mkuu huyo kuwa watafanyakazi kwa mashirikiano makubwa bila ya kujali vyeo vyao walivyonavyo.

“Tuko tayari kufanya kazi na wakubwa zetu kwa mashirikiano makubwa na wala hatutokuwa watoro, watu wa majungu na kila ambalo halifai kwenye kazi zetu za kila siku” alisema Khamis.

Katika hafla hiyo jumla ya wapiganaji 37 kutoka kambi ya Afisi kuuJKU Pemba walipandishwa vyeo kuanzia L/coplo hadi Wo1.

Post a Comment

0 Comments