Na Yussuf Hamad, Pemba
MFUKO wa Maendeleo ya jamii Tanzania Tassaf, umetoa jumla ya shilingi milioni 598,174,010 kwa ajili ya kutekeleza miradi 29 ya maendeleo ya wananchi kisiwani Pemba.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini kwake Chake Chake, mratibu wa Tassaf Pemba, Issa Juma Ali, alisema kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha, umekifanya kisiwa cha Pemba kutekeleza miradi
inayofikia 377 yenye thamani ya shilingi bilioni 6,072,640,616 tokea kuanza awamu ya pili.
“Tokea kuanza Tassaf II miaka mitatu iliyopita tayari miradi 377 imeshapatiwa fedha zaidi ya shilingi bilioni sita, kwa kweli ni faraja kubwa kwa wananchi wa kisiwa cha Pemba”, alisema Issa.
Mratibu huyo wa Tassaf, alitaja miradi hiyo iliyopatiwa fedha kuwa ni miradi ya barabara iliyopatiwa shilingi 79,911,040, ufugaji wa kuku wakienyeji iliyopatiwa shilingi 88,648,000, na ufugaji wa ng’ombe na mbuzi wa asili uliopatiwa shilingi 109,999,384.
Miradi mengine ni yakilimo cha umwagiliaji maji, iliyopatiwa shilingi 159,232,040, uvuvi shilingi 19,996,460, miradi ya upandaji miti shilingi 23,861,764 na miradi ya ujenzi wa matuta ya kuzuiya maji chumvi imepatiwa shilingi 89,984,070.
Alizitaja shehia zilizonufaika na miradi hiyo kumi, Jadida, Michungwani, Uweleni, Micheweni, Mjini Wingwi, Majenzi, Jombwe, Gando, Ukunjwi, Mvumoni, Kinowe, Chumbageni, Mtangani, Wingwi mtemani, Wawi,
Mchangamdogo, Ngwachani, Makangale, Mkoroshoni na Wara
0 Comments