Duka la Madawa la Izmir Mkunazini limeikabidhi Kamati ya Kuendeleza Michezo Zanzibar, msaada wa Madawa zenye thamani ya Shilingi milioni mbili, kwa timu za Jamuhuri na Mafunzo ili kuweza kushiriki vizuri katika Michuano ya Afrika inayotarajiwa kufanyika hivi karibu katika viwanja vya Gombani na Amaan..
Mkurugenzi wa Duka hilo la Madawa Nizar Abuu Machano, amesema ametowa mchango wake kwa timu hizo ili kuziwezasha timu hizo kufanya vizuri katika michuano inayozikabuili timu hizokuweza kufanya vizuri.
Amesema mchango huo ameutoa ili kuzipa changamoto timu hizo ziweze kufanya vizuri katika michezo yao ya awali inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni wakati timu ya Jamuhuri itacheza mchezo wake 18-2-2012 katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba, na timu ya WHAGE kutoka Zimbabwe.na mchezo mwengine utakuwa kati ya Mafunzo na Makurumano kutoka Msumbiji.19-2-2012, katika Uwanja waAmaan.
Amewataka Wafanyabiashara kujitokeza kuchangia timu zetu ili kuinuwa kiwango cha michezo katika Visiwa vya Zanzibar, na kjutowa changamoto kwa Vilabu mbalimbali kuweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje.
Ameitaka Kamati ya Kuendeleza Michezo Zanzibar isichoke na kazi yake iliopewa na ichukuwe juhudi za makusudi kufanikisha azma yao ya kuinuwa kiwango cha Michezo mbalimbali hapa Zanzibar nay eye yuka tayarui kutowa msaada kwa Kamati hiyo.
Nae Mwenyekiti wa Kamati hiyo Sharifa Khamis, ametowa shukrani kwa Duka hili la Madawa la Izmir, limetowa msaada wake wakati muafaka, ikizangatiwa na timu kuwa na majukumu makubwa inazozikabili wakati huu wa kushiriki mashindano hayo.
Amewata Wafanyabiashara wengine kujitokeza kutowa misaada kwa timu zao za Zanzibar ili kuzipa moyo na kuweza kushiriki vizuri katika mashindano yao na kumpongeza Mkurugenzi wa Duka la Madawa la Izmir Nazir Abuu Machano kwa msaada wake aliotowa kwa timu zetu za Jamuhuri na Mafunzo katika muda muafaka. Ambao timu hizo zinahitaji madawa katika kipindi hichi cha kujianda na michuano hiyo.
0 Comments