6/recent/ticker-posts

Ligi Kuu ya Zanzibar Haina Vipaji vya Kuitwa Timu ya Taifa?

Jana kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars alitaja kikosi chake cha wachezaji 23 kitakachovaana na Msumbiji kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) ambapo fainali zinatarajiwa kufanyika mwakani Afrika Kusini.

Katika kikosi alichokitaja kuna wachezaji kutoka Zanzibar kama Goli kipa Mwadini Ally, Abdi Kassim, Aggrey Morris (Azam) Masoud Cholo ( Simba) na Ally Badru ( Canal Suez, Misri)

Kitu ninachotaka tukikumbuke kwamba timu hii ya Taifa imeweza kuwaona wachezaji wanaocheza katika Timu zinazocheza ligi kuu Bara ambazo hushiriki ligi kuu pamoja na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.


Timu hii haina hata mchezaji mmojaambae anacheza katika ligi kuu Zanzibar ambae labda ameweza kufikia kiwango cha kuitwa katika ‘National team’

Suala. Je Zanzibarm, licha ya kuwa na ligi ambayo sasa inaendelea, haina wachezaji wa aina hiyo? Au ligi yetu ni ndogo na haina ushindani na hivyo hata wachezaji wetu huwa hawana uwezo wa si kupata namba tu hata kuitwa katika timu hii?

Wakati zamani Zanzibar na ligi yake hii hii chini ya uongozi wa michezo iliweza kutoa wachezaji na wengine kuwa na namba za kudumu na wala hawakuwa wakicheza katika timu za Bara kama kina Innocent Haule kaba ya kuhamia Simba, Ali Bushiri (Tanzania One Small Simba), Zahor Salum, Amour Aziz Kijeba(Malindi), Abdulwakati bin Juma, Leonard (Omar) William( Small Simba) , Juma Bakari Kidishi( Mlandege), Seif Bausi( Small Simba) na wengi wengineo.

Karibuni kulikuwa na mashindano ya Chalenji ambapo timu ya Zanzibar ilifanya vyema licha ya kutolewa robo fainali katika mashindano hayo ambapo iliweza kupambana na Sudan ambayo majuzi tu ilishiriki fainali za Kombe la Afrika. Poulsen hakuweza kuona vipaji vyovyote pale zaidi ya Ally Badru? Na Poulsen aliwahi kufanya ziara nchini Misri akamuona kijana wetu akikipiga au alitosheka na alivyomuona Chalenji?

Katika Mashindano ya Mapinduzi Cup yaliyofanyika mwezi uliopita tu tuliona timu za Zanzibar zilivyoweza kwenda sambamba na timu za Bara ambazo zenye majina hadi timu ya Jamhuri kutoka Pemba kufika fainali za mashindano yale na Azam. Hapakuwa na kipaji chochote pale?!

Kocha Poulsen huwa anakuja Zanzibar kuja kuona mashindano ya ligi kuu na kuangalia vipaji?

Viongozi wa michezo siwatarajii kulalamika kwa Kocha bali wanalionaje hili hasa katika Saikolojia ya wachezaji wetu ambao watajiona kuwa na inferiority complex na pia hawana thamani licha ya kujituma kwao na kuwa na malengo yao waliyojiwekewa kiuchezaji kama kuonekana wakicheza katika timu za nchi zao.

Je Zanzibar hatuna vipaji vyenye sifa ya kuitwa Timu ya Taifa?

Post a Comment

0 Comments