6/recent/ticker-posts

Mjini Yatinga Robo Fainali Copa Coca Cola

Na Ameir Khalid 

TIMU ya soka ya Mkoa wa Mjini Magharibi, imekata tiket ya robo fainali ya mashindano ya vijana Copa Coca Cola, baada ya juzi kuinyuka Manyara kwa magoli 2-1 katika uwanja wa Nyumbu Kibaha.

Huo ni ushindi wa tatu mfululizo kwa timu hiyo, huku ikitinga hatua hiyo, ikiwa imebakiwa na michezo mitatu mkononi. 

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutokea Kibaha, Katibu wa ZFA Wilaya ya Mjini Yahya Juma Ali, aliwataja wafungaji wa mabao hayo kuwa ni Salum Maulid na Juma Mohammed waliozifumania nyavu katika dakika za 30 na 40 mtawalia. 


 Nayo timu ya Mkoa wa Kusini Unguja, imemudu kuonja ladha ya ushindi kwa mara ya kwanza, baada ya kuwazamisha wenyeji Pwani kwa magoli 3-2, mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa Tamko Kibaha. 

Kocha Mkuu wa timu hiyo Salum Ali Haji, aliwataja wafungaji wa magoli hayo ambayo walipachikwa kiniani katika kila kipindi, goli la kwanza limefungwa na Omar Abdalla 15, wakati yale mawili yalifungwa kipidi cha pili na Kheri Ibrahim 80, kwa mkwaju wa penalt na goli la tatu liwefungwa na Ismail Ali 85, timu hiyo imbakiza michezo mitatu na endapo itashinda yote itaingia hatua ya 16. 

Kocha Mkuu wa timu hiyo Salum Ali Haji, aliwataja wachezaji walioitoa kimasomaso timu hiyo kuwa ni Omar Abdalla aliyefunga katika dakika ya 15, Kheri Ibrahim dakika ya 80 kwa mkwaju wa penelti, na Ismail Ali aliyefunga kitabu katika dakika ya 85.

Post a Comment

0 Comments